Skip to main content

Posts

Showing posts with the label kung'oka

Kupoteza Nywele baada ya Kujifungua Update (Bidhaa)....

Natumaini Post hii itakukuta ukiwa Mzima wa afya. Kama nilivyoahidi, leo nitakuelezea utaratibu wangu uliosababisha nywele(Relaxed) zangu kurudia Afya yake baada ya kuzipoteza na kupata "upara" wa muda. Jikoni kuna mwanga asilia, sihifadhi Bidhaa hizi Jikoni....hihihi! Ukiachilia mbali kuongeza aina ya Mboga iitwayo Kale kwenye Mlo wangu wa kila siku na kula Mayai 2-3 kila asubuhi. Bidhaa hizi zimechangia kwa kiasi kikubwa kuzuia Nywele zangu kuendelea kung'oka/anguka baada ya Kujifungua. Utaratibu wangu Rahisi. Kila Siku: Napaka Cantu Shea Butter kila siku asubuhi na Jioni na baada ya kupaka Cantu huwa na-"seal" na Mafuta asilia ya Sweet Almond. Kila Wiki: Huosha na Deep Condition Nywele zangu mara Moja (kila Ijumaa/JumaMosi) na huwa natumia Cream of Nature shampoo. Baada ya hapo nafanya deep condition kwa kutumia Vitale Mayonaise ambayo huwa nachanganya na Hello hydration (haipo pichani) na aina 2 za Mafuta asilia ambayo