Skip to main content

Posts

Showing posts with the label kujaji

Kukosoa na Kumcheka mtu ni "interest" yako?

Nakuona! Wengi huamini kuwa ukiwa na tabia ya kukosoa au kucheka watu wengine basi wewe utakuwa na Matatizo kwenye Maisha yako, maisha yakoo hayana furaha na yamejawa na Huzuni na hivyo kukosoa na kucheka watu ndio njia pekee ya kujipatia "furaha". Nakubali kwa kiasi fulani, kwa baadhi kuwa Hasi kwenye kila kitu  ni tatizo na linaathiri maisha yao ya kila siku. wengine huamua kuwa Hasi kama sehemu ya kupata "attetion" au "Trafic" na "Views" popote walipo kwenye Sosho Midia. Kwa wale wa Ughaibuni, Maisha mitaa hii yanaweza kuwa ya Upweke sana na hivyo kumfanya mtu kutumia muda wake mwingi kwenye kutafuta "furaha" kwa kuwa Negative towards watu wengine. Upweke wa huku unatokana na utofauti wa Kitamaduni, Utaratibu wa kazi za "shift",  Majira ya Mwaka(Kiza kuingia mapema) vilevile kutumia muda mwingi kusafiri to na from work....by the time unafika nyumbani upo hoi, tayari ni Giza hivyo  hakuna muda wa kutoka au kukarib

Weusi wa Ngozi sio Uchafu....

....ila usipokuwa muangalifu kwenye kuchagua Rangi za Mavazi/Nywele hakika utaonekana Mchafu(huvutii), hii  haina kujiamini.....nadhani ni muhimu kuchagua Rangi zinazoendana na Rangi ya Ngozi  yako. Mambo?!! Kuna siku nipo na mishughuliko yangu ya ndani wakati Asali wa Moyo anatazama Mashindano ya Tenesi ya Wibledoni. Anapendezwa sana na wale Williams Dadaz....mmoja wao alikuwa anacheza. Mwenyewe anafurahia uchezaji wake (au kuona Tako  kila kisketi chake kinapoinuka hihihihi maana mdada mMashallah). Sina hili wala lile nasikia mwenznagu anawasifia wadada Williams kwa kutokuwa kama Celebs wengine.....mie nkasema hao sio ma-Celeb ni Sports Stars (kwa Kiswahili ndio tunasemaje vile?) ila Media inalazimisha kuwaweka kwenye Kundi la M-aceleb kitu ambacho sio haki kwasababu wapo walipo kutokana na kazi/kujituma kwaoo na sio kuonekana kwenye Tv au kuuza Haidthi kwenye magazeti au....oh well kwa Umalaya. Katika kufunga maelezo yangu nikamalizia na....kiukweli mie siwaelewi