Skip to main content

Posts

Showing posts with the label wenyendoa

Wenye Ndoa, tuache kuwabadilisha Waume Zetu.

Sasa kabla hatujaanza kumsimamnga Wifi kambadilisha Kaka yetu, tuangalie kwanza Wifi alikuwa nani kwao, na je uamuzi wa Wifi kupumzika ki-career baada ya Kuzaa ni kum-support Kaka yenu(Mumewe) ki-career au ni njia tu ya yeye kula Mahela ya Kaka yenu? Je ndugu zake waliokuwa wakimtegemea hawateseki kwa kukosa "kipato" kutoka kwa Dada/Mwana wao? Kwenye era hii ya Sosho Midia inabidi uwe makini sana maana info ni za kumwaga(tofauti na 2007 nilipoanza  kublog), ni kweli baadhi zinasaidia hasa zile za Medical kutoka kwenye Site za Shirika la Ugojwa husika au Shirika la Afya Duniani. Lakini linapokuja suala la Ndoa au mahusiano, ongeza umakini kwasababu Ndoa hazina Kanuni Moja na watu hatufanani hata kama tulikaa tumbo Moja Miezi 9 na kuzaliwa kupitia Njia mooja na siku Moja bado tutatofautiana kwa kiasi fulani. Maisha magumu, kila mtu anatafuta views na clicks siku hizi, mara zote(kama Wanasiasa) watu huamua kuongea au kuandika mambo ambayo wanajua watu watakuja mbio ku