Morning/Noon!
Lugha za Tanzania zinaingiliana hivyo hazikeri alafu lazima utaambulia maana kwa mbali hasa kama unatetwa.
Kuna Mtangazaji "Tiger beibiiii" wa Ebony ya Iringa huwa ananikosha sana akitumbukizia/nogesha kwa kilugha chake, sio Watangazaji wa Dar wamejaa "you know what I mean" "waraaaap" nyiingi....hiyo sio nukta, nimegusia tu.
Lugha za Nchi hii bana ayee! Kichina, Kinigeria, Kipolishi, Kizairwaa, Kisomali, Kirusi na nyingine nyingi....zinakera sana (kwasababu sing'amui kitu).
Asa ombea umepanda Basi Moja na Mnaija, Mkongo na Mchina, alafu wapigiwe simu kwa wakati mmoja....Utadhani wamekodisha basi kwa ajili yao tu.
Sikuhizi nawaelewa sana Wainglishi wanapoonyesha kukerwa unapoongea Kilugha chako....(Sehemu ni wivu as hawajui lugha nyingine hihihihihi).
Huwa siongei Kiswahili ninapokuwa kwenye kadamnasi ya watu ambao najua hawaelewi na kama mazungumzo ni nyeti (lazima kilugha ili wengine wasielewe) basi huwa naahidi kurudisha simu bidaae.
Sio kwamba naona haya au sijivunii Lugha yangu Kiswahili (herooo naandika kwa kiswanhehe hapa araa)...la hasha! Sipendi kuwa "rude" kwa watu wengine.
Changamoto nyingine ni Mwanangu mkubwa, yaani sina raha na Kilugha (Kiswahili) changu humu ndani....nikiwa naongea Kijana analia utafikiri kakatwa sikio huku anasema "mummy that is not Englis, Englis please"
Englis ndio English....
Kwaheri kwa sasa.
Mapendo tele kwako...

Comments