Skip to main content

Kesi za Kubaka za Miaka ya 70s-80s....

Bari gani?


Hizi Kesi na Hukumu zinazotolewa huku dhidi ya "vibabu" waliobaka au ku-abuse wasichana wadogo miaka 40 iliyopita zinaudhi eti!



Unaeza sema "masikini vibabu vya watu vinafungwa bure kwa makosa ya miaka ile".....au ukajiuliza "hao wanawake walikuwa wapi tangu enzi zile kupeleka Mashtaka yao".



Well! Huwezi kuelewa mpaka uwe umepitia huko au wewe ni mwanamke na unakuwa targeted kwasababu tu una Matiti na Uke.




Sipendi kulinganisha lakini linapokuja suala la ku-abuse wanawake kingono hasa sehemu za kazi Tz, mimi ni mmoja kati ya wengi ambao tulitishiwa kufukuzwa (kunyimwa ajira ya Kudumu) kama tutakataa kujitoa kimwili.




Wenzangu sijui, lakini mie na misimamo yangu nikamwambia "unikome ka' ziwa la mama yako na sina shida na Kazi yako".....nikatoka, mefika nyumbani nikaenda kumshitaki kwa Mama na Baba (hihihihi hapo nilikuwa Binti wa miaka 25).




Sijui sheria ya Unyanyaswaji wa Kijinsia na Ubakaji ilivyo Tanzania, ila ingezingatiwa na wahusika kufuatilia kesi za namna hiyo ingekuwa vema sana.




Si Uinglishini tu bali kila mahali Duniani. Imekuwa tabia ya walio kwenye "nafasi" fulani kunyanyasa wenye mahitaji ya kupata kazi au kupanda cheo.




Wake kwa waume wanafanya uchafu huo, lakini wanaume wanaongoza. Ingewezekana watu tukaitwa kutoa maushahidi ya Ushenzi wa watu sehemu za kazi ili wafungwe ingependeza sana.




Jamaa (sex abusers) mmoja yupo Ikulu sasa hivi na Mwingine amekuwa mwanaharakati hihihihiihihi Possibly bado wanatishia watu(they are both ill, well Old).




Wasichana walikuwa wanajitolea kwao na kuishia kulalamika na kujipa matumanini "sasa tufanyeje na kazi tunaitaka" aiiiii Elimu yangu na utendaji wangu utanipatia kazi, sio mwili wangu.




Anyway....kuna majamaa nawasubiri hapa tangu saa mbili, hawajaonekana mpaka sasa (saa Nane).



Kuna zile ahadi za "nitakuja kati ya saa Mbili na Saa kumi jioni" unazijua? Yaani unapotezewa siku nzima kumsubiri mtu ambae huna uhakika atakuja mida gani?



Nikuache kwa sasa....
Mapendo tele kwako...

Comments

Topic hizi tamba...

Weusi wa Kwapa na Vipele Makalioni....

Well Weupe huwa hawawi na weusi kwapani bali Unjano au Ukahawia....wale wenye nywele nyeusi sasa ni another case. Kuhusu Vipele makalioni havina Ubaguzi, raha ya vipele vile ni kwamba havionekani kwa Macho....utajua unavyo kwa kujipapasa, au gusa ngozi yako....inakuwa kama ina "mikwaruzo" wajua ile nanihii ya kupiga Msasa mbao? Yep ndio feels kama hivyo! Usione haya sio Ugonjwa na wala sio Tatizo kiafya, ni mambo ya Urembo tu na yawapata watu mbali mbali Ulimwenguni.....kama urembo sio issue kwako basi baki na Mapele yako na uyafurahie! Mimi nilikuwa nayo na siyapendi na ndio maana nataka nikupe mbinu ya "mapambano" ili uwage na Makalio "smooth"....Sasa hapa nikuambie kuhusu Vipele Makalioni au weusi wa Kwapa?.....Yote? Hamna shida twende in to them*. Vipele: Sijui inasababishwa na nini(sio mtaalam mie) ila nahisi ni kutoijali ngozi ya sehemu hiyo ndio inachangia....huisugui ukioga, huilainishi kwa mafuta, unavaa chupi za Mpira badala ya Pamba, huifanyishi

Kuachisha mtoto Kunyonya!

Heeeeeelp!!! Ka Binti kangu kana Mwaka na Nusu (Miezi18) lakini kamo tu, hata dalili ya kuacha hakana....Mie nimechoka kunyonyesha, nimechoka kuwa Mkubwa hapa Chini ya Kidevu bana! Babuu aliacha mwenyewe ghafla, yaani siku hiyo kaamka tu akagoma kunyonya....Mwanamke bembeleza, lazimisha mtoto wapi!!....alikuwa na Mwaka Moja na Mwezi(Miezi 13) na niliteseka Kihisia na Kimwili kwa Wiki nzima. Kihisia: Haina Uzungu hii, ila nililia sana....kwanini Mwanangu hataki kuwa karibu na mimi? (maana kunyonya kwake kulikuwa kunanipa ukaribu na Mwanangu). Nilipanga kumnyonyesha mpaka Mwaka na nusu (Miezi 18), kwanini Kanigaya(Susa) kabla sijawa tayari?!!! Kimwili: Matiti yanauma bwana asikuambie Mutu! Yalivimba(Jaa maziwa)....the more nakamua ndio yanajaa zaidi.....kamata simu Pigia Mama, Mama akasema "usiyakamue kwani ukikamua mwili wako unahisi mtoto anataka kunyonya zaidi so yanajitengeneza kwa Kasi ya ajabu". Kaongeza: "

Mashoga/Wasenge "wanatuibia" Waume/Wapenzi wetu....

...kwanza kabisa napenda utambue kuwa hakuna Mtu anaweza kumuiba  mwenzake kimapenzi, Mpenzi wako anapotoka kwako na kwenda kwa mwingine ni wazi kwamba kaamua kufanya hivyo, hilo sio kosa lako na wala hujasababisha yeye kwenda huko kwingine bali ni yeye mwenyewe na akili zake timamu kafanya uamuzi huo. Tangu Ushoga ndio khabari/Suala Muhimu wacha na mimi nidaivu ini nipate "trafiki" japo nimechelewa. Tofauti na "platform" nyingine hapa utajifunza kwa kiasi kidogo...au niseme kiasi fulani. Linapokuja suala la Ushoga/Usenge,sehemu kubwa ya Jamii imetawaliwa na  Uoga ambao unapelekea kutokuelewa Ushoga ni nini? Hali hiyo ni Asilia, kwamba mtu anazaliwa hivyo au ni uamuzi  wa mtu au ni Hali inayojitokeza ukubwani baada ya Kubalehe.....pale kijana anapoanza kutambua ujisia wake(je anavutiwa/penda Wanawake au Wanaume au wale wa Jinsi kama yake). Mie sio Mtaalam wa Masuala ya Kisenge/Shoga lakini ni mtu ambae napenda kudadisi, na watu wazuri kuwadadisi ni hao hao