...well, inategemea na unachokifanya for a living sio! Si unajua ile Kuapa au kuweka sahihi kuwa kamwe hutotoa siri (ujuayo) ya Kampuni/Mgonjwa/Mteja n.k. isipokuwa tu ikiwa Serikali na Mahakama itahitaji. Hello, natumaini Post hii imekukuta ukiwa na afya njema.
Mie binafsi naamini kuwa kutunza "siri" ya mtu au watu ni wajibu wako. Kutokana na kile nilichokuwa nikifanya Miaka 8 iliyopita baadhi ya watu walijenga Uaminifu kwangu, kwamba walikuwa huru kuniambia mengi kuhusu wao na maisha yao. Kwa maana hiyo nafahamu mengi ya watu wengi ambao hatufahamiani.
Ile ilikuwa "kazi" ya kujitolea, sijasomea nilichokuwa n akifanua isipokuwa nilitumia uelewa wangu na uzoefu wangu(natambua unalijua hilo), hivyo sikula Kiapo na wala sikutia saini kuwa nitabaki na "siri" za watu Milele(haina maana nitazitoa).
Pamoja na kuwa hakuwa "Kazi" bado nilichukulia na ninaendelea kuchukulia kuwa ni wajibu wangu kuto-share chochote kuhusu watu wote walioniandikia na hata wengine kuongea nami kwa Simu, bila kusahau wale niliobahatika kukutana nao.
Pamoja na kusema hivyo haina maana huwa nakaa na kuanza kurudia mails zao au kufikiria ninayoyajua kuhusu wao kama Wenza au kama Mwanaume/Mwanamke. Sasa ili kuondoa "mzigo" nilikuwa na kawaida ya kufuta mails mara baada ya mhusika kurudisha feedback.
Kwa wale ambao bado naendelea kuonana nao "online" ni wazi kwamba nikiwaona nakumbuka aah huyu alikuwa na hili na lile, aah yule aliniambia ana hili na lile. Hii hunifanya nihisi kuwa pengine hawa watu wanaweza kuwa na wasiwasi kuwa siku moja Dinah atakuja kusema niliyowahi kumuambia kuhusu mimi na fulani.
Lengo la Post hii ni kukusaidia uwe na Amani, usinikwepe(hihihihihi) sijawahi na Kamwe, KAMWE sito-share ulichowahi kunielezea. Ni wajibu wangu kuachana na uliyoniambia kama nilivyoachana na Blog iliyokufanya utake Ushauri wangu.
Sio kwamba sijawahi kutoa siri, nimewahi kutoa siri na sababu kuu ya kuitunza ilikuwa kutoonekana "wifi/shemeji" mgomvi. Lakini baada ya miaka Mingi Ndoani nikajua mengi kuhusu Jamaa niliekuwa namtunzia Siri against Cuz yake(mume wangu), so nikaitoa.....hihihihi the man is my husband. Sina siri kwa Mume wangu ayee!
Heey....naheshimu na kuthamini Muda wako mahali hapa, ahsante kwa kuichagua Blog hii.
Babai.
Comments