Skip to main content

Posts

Showing posts with the label ukweli

Kutunza Siri ni Wajibu wako....

...well, inategemea na unachokifanya for a living sio! Si unajua ile Kuapa au kuweka sahihi kuwa kamwe hutotoa siri (ujuayo) ya Kampuni/Mgonjwa/Mteja n.k. isipokuwa tu ikiwa Serikali na Mahakama itahitaji. Hello, natumaini Post hii imekukuta ukiwa na afya njema. Mie binafsi naamini kuwa kutunza "siri" ya mtu au watu ni wajibu wako. Kutokana na kile nilichokuwa nikifanya Miaka 8 iliyopita baadhi ya watu walijenga Uaminifu kwangu, kwamba walikuwa huru kuniambia mengi  kuhusu wao na maisha yao. Kwa maana hiyo nafahamu mengi ya watu wengi ambao hatufahamiani. Ile ilikuwa "kazi" ya kujitolea, sijasomea nilichokuwa n akifanua isipokuwa nilitumia uelewa wangu na uzoefu wangu(natambua unalijua hilo), hivyo sikula Kiapo na wala sikutia saini kuwa nitabaki na "siri" za watu Milele(haina maana nitazitoa). Pamoja na kuwa hakuwa "Kazi" bado nilichukulia na ninaendelea kuchukulia kuwa ni wajibu wangu kuto-share chochote kuhusu watu wote walion