Skip to main content

Addicted to Dini....

Jiadhari, inaua!


Wataalamu wanaamini kuwa kila Mwanadamu anaumwa Akili(anaugonjwa fulani wa Akili) na huwa triggered na aina ya Maisha anayoishi mhusika.




Sasa kuna wale watu wako so dedicated na Imani zao mpaka unahisi akili zao hazipo sawa....hizo mtu zipo Addicted (Dini imetriga Gonjwa la Akili).




Kama zilivyo addictions nyingine Imani ya Dini inaharibu Mahusiano, Inasababisha Mfarakano kati ya familia na familia na hatimae kupoteza Maisha au kumfanya Muathirika kuishi Maisha yale yale wakati Mkuu wa Dini (Zungu) anafurahia the High life + attention ya Jamii.





Nakumbuka enzi, Mtu (kwenye familia yangu) alikuwa yupo radhi kupeleke "fungu la Kumi" kanisani kila Mwezi kuliko kuwanunua watoto wake mahitaji muhimu.




Ilifikia mahali anasomesha watoto wa Waumini wengine wakati Elimu ya watoto wake haieleweki.




Addiction ilinoga akaamua kuacha kazi ili "afanye kazi ya Bwana"....akawa anaamka asubuhi kwenda Kanisani na kurudi jioni (kama alivyokuwa akifanya kazi).




Alikesha akiomba, alifunga na kuomba for weeks mpaka anakondeana na kushindwa kutembea...ndio anafungulia. Akipata nguvu anafunga tena hehehehehe Magonjwa ya akili yaja in every form and shape, I tell you.




Kuna wale wajao kwenye Blog ile nyingine na kuweka maelezo ya "addiction" zao kwenye Comments which huwa nazidharau.




"Hilo ni tatizo dogo sana, Mgeukie Mungu atakusaidia, atamrudisha Mkeo/Mumeo....kwa Maombi piga namba hii"....



"Kwa maombi ya kuoa au kuolewa haraka, niandikie" yeah right "Zungu la Dini" tafuta supplier Mwingine....!




Waliotuletea Dini wanasema Mungu yupo kwa ajili ya kukupa Comfort (kuongea mwenyewe ukiamini unasikilizwa bila kujibiwa ni therapy)....Juhudi zako, Kujiamini kwako kuwa utaweza na utafanikisha ndio kunafanikisha Mambo.....*whispering* Sio Mungu.



Namuamini Mungu, ni sehemu muhimu ya Maisha yangu....lakini!!!

Babai...
Mapendo tele kwako...

Comments

Topic hizi tamba...

Weusi wa Kwapa na Vipele Makalioni....

Well Weupe huwa hawawi na weusi kwapani bali Unjano au Ukahawia....wale wenye nywele nyeusi sasa ni another case. Kuhusu Vipele makalioni havina Ubaguzi, raha ya vipele vile ni kwamba havionekani kwa Macho....utajua unavyo kwa kujipapasa, au gusa ngozi yako....inakuwa kama ina "mikwaruzo" wajua ile nanihii ya kupiga Msasa mbao? Yep ndio feels kama hivyo! Usione haya sio Ugonjwa na wala sio Tatizo kiafya, ni mambo ya Urembo tu na yawapata watu mbali mbali Ulimwenguni.....kama urembo sio issue kwako basi baki na Mapele yako na uyafurahie! Mimi nilikuwa nayo na siyapendi na ndio maana nataka nikupe mbinu ya "mapambano" ili uwage na Makalio "smooth"....Sasa hapa nikuambie kuhusu Vipele Makalioni au weusi wa Kwapa?.....Yote? Hamna shida twende in to them*. Vipele: Sijui inasababishwa na nini(sio mtaalam mie) ila nahisi ni kutoijali ngozi ya sehemu hiyo ndio inachangia....huisugui ukioga, huilainishi kwa mafuta, unavaa chupi za Mpira badala ya Pamba, huifanyishi

Kuachisha mtoto Kunyonya!

Heeeeeelp!!! Ka Binti kangu kana Mwaka na Nusu (Miezi18) lakini kamo tu, hata dalili ya kuacha hakana....Mie nimechoka kunyonyesha, nimechoka kuwa Mkubwa hapa Chini ya Kidevu bana! Babuu aliacha mwenyewe ghafla, yaani siku hiyo kaamka tu akagoma kunyonya....Mwanamke bembeleza, lazimisha mtoto wapi!!....alikuwa na Mwaka Moja na Mwezi(Miezi 13) na niliteseka Kihisia na Kimwili kwa Wiki nzima. Kihisia: Haina Uzungu hii, ila nililia sana....kwanini Mwanangu hataki kuwa karibu na mimi? (maana kunyonya kwake kulikuwa kunanipa ukaribu na Mwanangu). Nilipanga kumnyonyesha mpaka Mwaka na nusu (Miezi 18), kwanini Kanigaya(Susa) kabla sijawa tayari?!!! Kimwili: Matiti yanauma bwana asikuambie Mutu! Yalivimba(Jaa maziwa)....the more nakamua ndio yanajaa zaidi.....kamata simu Pigia Mama, Mama akasema "usiyakamue kwani ukikamua mwili wako unahisi mtoto anataka kunyonya zaidi so yanajitengeneza kwa Kasi ya ajabu". Kaongeza: "

Mashoga/Wasenge "wanatuibia" Waume/Wapenzi wetu....

...kwanza kabisa napenda utambue kuwa hakuna Mtu anaweza kumuiba  mwenzake kimapenzi, Mpenzi wako anapotoka kwako na kwenda kwa mwingine ni wazi kwamba kaamua kufanya hivyo, hilo sio kosa lako na wala hujasababisha yeye kwenda huko kwingine bali ni yeye mwenyewe na akili zake timamu kafanya uamuzi huo. Tangu Ushoga ndio khabari/Suala Muhimu wacha na mimi nidaivu ini nipate "trafiki" japo nimechelewa. Tofauti na "platform" nyingine hapa utajifunza kwa kiasi kidogo...au niseme kiasi fulani. Linapokuja suala la Ushoga/Usenge,sehemu kubwa ya Jamii imetawaliwa na  Uoga ambao unapelekea kutokuelewa Ushoga ni nini? Hali hiyo ni Asilia, kwamba mtu anazaliwa hivyo au ni uamuzi  wa mtu au ni Hali inayojitokeza ukubwani baada ya Kubalehe.....pale kijana anapoanza kutambua ujisia wake(je anavutiwa/penda Wanawake au Wanaume au wale wa Jinsi kama yake). Mie sio Mtaalam wa Masuala ya Kisenge/Shoga lakini ni mtu ambae napenda kudadisi, na watu wazuri kuwadadisi ni hao hao