Skip to main content

Posts

Showing posts with the label fat

Come to terms with your Uchibonge....

Hello! Naweka viraka mbinguni ujue(mekuwa busy namna hiyo). Mwisho wa wiki nilipata wasaa wa kupekua pekuwa YouTube na huko nikakutana na "how to gain weight".....nikabofya na kuanza kusikiliza hadithi moja baada ya nyingine kuhusu Wanawake wanaotaka sana kunenepa. Unajua unapomsikiliza mtu au kusoma hadithi yake na kuhisi kuwa anakysemea au kukuwakilisha wewe? Yaani anakugusa kumtima. Nikakumbuka jinsi nilivyokuwa Chikonda (skinny)enzi zile nakua(nimeacha kukua nilipofikisha miaka 25 nadhani). Story Time: Nilikuwa mwembamba kiasi kwamba baadhi ya watu walidhani nina Ugonjwa. Mmoja wa Binamu zangu alikuwa akiniambia "mtu mwenyewe maiti wewe.....umebaki mifupa tu". Nilipofika late teen baadhi ya watu Familiani wakawa wanasema ninatoa mimba sana wakati sikuwa namjua mwanaume sasa sijui Mimba ziliingia kwa Roho mtakatifu! Wengine walisema naiga Uingilishi figa na hivyo kutumia madawa ya kujikondesha. Nilichoka kusakamwa kwa uchikonda wangu ambao sikuuom