....ndio tulipokea kwa nguvu zote suala la Haki za Mwanamke au Usawa aka U-Beijin. Waliopigana vita ni Mama zetu ambao hawakutaka sisi tuonewe kama ambavyo wao walionewa. Baadhi ya Mama zetu hao walikuwa na Hasira na Wanaume kutokana na "treatment" walizopatiwa na Wanaume kama Wenza wako, Wafanya kazi wenzao, Wakubwa wao kwenye Familia na Maboss wao.
Ujumbe na maana na nia ya "Ubeijing" ilikuwa nzuri na bado ni nzuri, lakini kwa baahati mbaya kwa baadhi ya akina Mama zetu hao waliziwakilisha kwetu, wasichana ambao tulizaliwa mwishoni mwa miaka ya 70s na 80s ambao ndio tumekulia era ya "Ubeijing" au niseme Miaka ya 90.
Heka heka za kupigania Haki/Usawa kwa wanawake imeanza miaka ya 60s kwa nchi niliyopo na mafanikio makubwa yalikuwa ni kutambuliwa kwa "haki" ya mwanamke kufurahia tendo la kufanya Mapenzi, kwamba tendo hili sio kwa ajili ya kumfurahisha mwanaume. Baada ya hapo ikaja suala la kutumia Kinda Dhidi ya Mimba(Kidonge).
Mkutano wa Nne wa wanawake uliofanyika Ubeijing mie nilikuwa ndio namalizia Shule ya Secondary. Nilikuwa najivunia sana ile Hotuba ya yule Mama wa Kitanzania (nimesahau jina lake na sina mpango wa kuGugo....soma Picha hihihihi) niliona kuwa ni Mwanamke Msomi(academically smart), Shupavu na Imara.
Sasa, sisi Wasichana wa Era hiyo ndio tulikuwa wa kwanza kuweka "Ubeijing" kwenye actions kwa nguvu zote.....tulikuwa kwenye "presha" bila kujijua, tulihakikisha tunabaki shule kwa muda mrefu (sio kukimbilia kuolewa) na kuipata hiyo Elimu kama Wanaume, Era hiyo wengi wetu tulichukua Masomo ya "Magumu" kama vile Sayansi(nili drop katikati though usicheke), tunafanya kazi za Ufundi,Uinjinia, Urubani,Ukandarasi n.k.
Wasichana wengi tulifaulu Mitihani, hatukuwa wa kati wala mwisho tena. Tuliongoza Darasa na Mikondo. Dhamira yetu ya kujitegemea na kuongoza na kuelimisha Jamii iliendelea kukua tulipopatiwa Mawaziri wa Kike na kuona Wakurugenzi(akina Ms Mhavile and co) wakifanya mambo.
Fast Foward:...kwa Wasichana wa leo(waliozaliwa 90s wamekulia 2000s) ambao wengi wanaumri kama ule wetu miaka ya 90, ni teens au wapo early 20s.....hawa are so relaxed! Wanajua haki zao, wanajua wanapaswa kujitegemea na how.....yaani kila kitu kipo wazi kwao hivyo hawapigani ile sanaa kama sisi miaka ya 90s.
Ni kama vile wameona "Ubeijing" haujafanikiwa kama tulivyotegemea(well tangu 1965 bado Wanawake hatujafanikiwa...safari ni ndefu). Wengi wa Era hii(2000s) wapo tayari kufanya kazi nusu siku ili wapate muda wa kuwa na Familia zao na kuachia Jukumu la Mume kubaki palepale. "Ubeijing" umefanya Baadhi ya Wanaume kuwa tegemezi na matokeo yake mwanamke anafanya Jukumu la Baba na Majukumu yake kama Mama. Wasichana wa 2000s wanachangamoto ya kubadilisha hili.
Wasichana wa 2000s(wanaokulia Era hii) wameanikiwa(wekea wazi) kila kitu na wao wana-choose and pick, tofauti na sisi ambao hatukupewa Option kwasababu tulikuwa hatujui lolote kuhusu nafasi ya Mwanamke kwenye jamii ambayo ni zaidi ya Kuzaa na Kulea watoto.
Natambua wanawake wengi walikuwa wakijituma na kuongeza Kipato kwenye familia kabla ya miaka ya 90(Ubeijing era) lakini bado hawakuwa na sauti au nguvu kwenye Vipato vyao, so ni kama walikuwa "watumwa" wa Wenza wao.
Naheshimu na kuthamini Muda wako hapa, Ahsante kwa kuichagua Blog hii.
Babai.
Comments