Skip to main content

Posts

Showing posts with the label miakaya90

Wasichana tuliokulia miaka ya 90...

....ndio tulipokea kwa nguvu zote suala la Haki za Mwanamke au Usawa aka U-Beijin. Waliopigana vita ni Mama zetu ambao hawakutaka sisi tuonewe kama ambavyo wao walionewa. Baadhi ya Mama zetu hao walikuwa na Hasira na Wanaume kutokana na "treatment" walizopatiwa na Wanaume kama Wenza wako, Wafanya kazi wenzao, Wakubwa wao kwenye Familia na Maboss wao. Ujumbe na maana na nia ya "Ubeijing" ilikuwa nzuri na bado ni nzuri, lakini kwa baahati mbaya kwa baadhi ya akina Mama zetu hao waliziwakilisha kwetu, wasichana ambao tulizaliwa mwishoni mwa miaka ya 70s na 80s ambao ndio tumekulia era ya "Ubeijing" au niseme Miaka ya 90. Heka heka za kupigania Haki/Usawa kwa wanawake imeanza  miaka ya 60s kwa nchi niliyopo na mafanikio makubwa yalikuwa ni kutambuliwa kwa "haki" ya mwanamke kufurahia tendo la kufanya Mapenzi, kwamba tendo hili sio kwa ajili ya kumfurahisha mwanaume. Baada ya hapo ikaja suala la kutumia Kinda Dhidi ya Mimba(Kidonge).