Skip to main content

Nguzo 5 za Mahusiano bora(Masikilizano/Maelewano).

Masikilizano/elewano huja wakati/baada ya mawasiliano japo ni Nguzo inayoweza kusimama peke yake kutegemea na tukio....mf:- wakati wa manunuzi makubwa(gari, nyumba), familia yenu iwe na watu wangapi?, Shule/Malezi ya watoto na pengine “career”.



Unapowakilisha jambo/kero kwa mwenza wako ni vema kuwa katika hali ya utulivu(sio mara zote hufanya kazi hasa kama mwenzio sio msikilizaji mzuri). Utulivu wako husaidia kutoongea kwa sauti ya kushambulia na hivyo kuepeuka yeye kujitetea(bila shambulio hakuna pa kurudisha shambulio).



Unapoibua suala ili lizungumzwe/jadiliwe nia ni kufikisha Ujumbe/kero na kupata muafaka(maelewano) na sio kung'aka na kuanza kugombana....hii hupoteza muda(kusumbua watoto kihisia/akili) na tatizo kuzimishwa badala ya kumalizwa.



Kuzima/acha tatizo bila muafaka/maelwano kwa muda mrefu hupelekea mwanzilishi wa “mazungumzo" kuhisi kuwa hasikilizwi na hisia zake hazithaminiwi na mwenza wake.



Hisia hizo hupelekea hasira(jitahidi kujizuia ili usifanye jambo mbaya) na pengine kupunguza Heshima kwa mwenza wake.


Kutoelewana/sikilizana pia hupelekea “issues" kurundikana kitu ambacho sio afya kwenye Uhusiano wenu.



Suala muhimu hapo ni Msikilizaji ambae hakusikiliza na badala yake kuanza kujitetea kwa kung'aka(na kutimia maneno  makali ya kuudhi) au kupuuzia na kuzima(kaa kimya) kuomba radhi.



Siku nyingine, jaribu kuomba mzungumze na kumwambia mwenza wako kuwa “naomba tuongee kuhusu bla-bla-bla, usikilize kwanza mpaka mwisho bila kufoka, kujibu wala kunikatisha.



Heshima ikikosekana kwa pande zote mbili, Uhusiano unaweza kuyumba na pengine kufa. Heshima ni Moja ya Nguzo muhimu sana pande zote mbili. 



Njoo tena ukipata muda, tuiangalie Heshima kwa “engo” tofauti na ile ya 2015.....Muda wako unathani kubwa kwangu, ahsante.
Bai.

Comments

Topic hizi tamba...

Weusi wa Kwapa na Vipele Makalioni....

Well Weupe huwa hawawi na weusi kwapani bali Unjano au Ukahawia....wale wenye nywele nyeusi sasa ni another case. Kuhusu Vipele makalioni havina Ubaguzi, raha ya vipele vile ni kwamba havionekani kwa Macho....utajua unavyo kwa kujipapasa, au gusa ngozi yako....inakuwa kama ina "mikwaruzo" wajua ile nanihii ya kupiga Msasa mbao? Yep ndio feels kama hivyo! Usione haya sio Ugonjwa na wala sio Tatizo kiafya, ni mambo ya Urembo tu na yawapata watu mbali mbali Ulimwenguni.....kama urembo sio issue kwako basi baki na Mapele yako na uyafurahie! Mimi nilikuwa nayo na siyapendi na ndio maana nataka nikupe mbinu ya "mapambano" ili uwage na Makalio "smooth"....Sasa hapa nikuambie kuhusu Vipele Makalioni au weusi wa Kwapa?.....Yote? Hamna shida twende in to them*. Vipele: Sijui inasababishwa na nini(sio mtaalam mie) ila nahisi ni kutoijali ngozi ya sehemu hiyo ndio inachangia....huisugui ukioga, huilainishi kwa mafuta, unavaa chupi za Mpira badala ya Pamba, huifanyishi

Kuachisha mtoto Kunyonya!

Heeeeeelp!!! Ka Binti kangu kana Mwaka na Nusu (Miezi18) lakini kamo tu, hata dalili ya kuacha hakana....Mie nimechoka kunyonyesha, nimechoka kuwa Mkubwa hapa Chini ya Kidevu bana! Babuu aliacha mwenyewe ghafla, yaani siku hiyo kaamka tu akagoma kunyonya....Mwanamke bembeleza, lazimisha mtoto wapi!!....alikuwa na Mwaka Moja na Mwezi(Miezi 13) na niliteseka Kihisia na Kimwili kwa Wiki nzima. Kihisia: Haina Uzungu hii, ila nililia sana....kwanini Mwanangu hataki kuwa karibu na mimi? (maana kunyonya kwake kulikuwa kunanipa ukaribu na Mwanangu). Nilipanga kumnyonyesha mpaka Mwaka na nusu (Miezi 18), kwanini Kanigaya(Susa) kabla sijawa tayari?!!! Kimwili: Matiti yanauma bwana asikuambie Mutu! Yalivimba(Jaa maziwa)....the more nakamua ndio yanajaa zaidi.....kamata simu Pigia Mama, Mama akasema "usiyakamue kwani ukikamua mwili wako unahisi mtoto anataka kunyonya zaidi so yanajitengeneza kwa Kasi ya ajabu". Kaongeza: "

Mashoga/Wasenge "wanatuibia" Waume/Wapenzi wetu....

...kwanza kabisa napenda utambue kuwa hakuna Mtu anaweza kumuiba  mwenzake kimapenzi, Mpenzi wako anapotoka kwako na kwenda kwa mwingine ni wazi kwamba kaamua kufanya hivyo, hilo sio kosa lako na wala hujasababisha yeye kwenda huko kwingine bali ni yeye mwenyewe na akili zake timamu kafanya uamuzi huo. Tangu Ushoga ndio khabari/Suala Muhimu wacha na mimi nidaivu ini nipate "trafiki" japo nimechelewa. Tofauti na "platform" nyingine hapa utajifunza kwa kiasi kidogo...au niseme kiasi fulani. Linapokuja suala la Ushoga/Usenge,sehemu kubwa ya Jamii imetawaliwa na  Uoga ambao unapelekea kutokuelewa Ushoga ni nini? Hali hiyo ni Asilia, kwamba mtu anazaliwa hivyo au ni uamuzi  wa mtu au ni Hali inayojitokeza ukubwani baada ya Kubalehe.....pale kijana anapoanza kutambua ujisia wake(je anavutiwa/penda Wanawake au Wanaume au wale wa Jinsi kama yake). Mie sio Mtaalam wa Masuala ya Kisenge/Shoga lakini ni mtu ambae napenda kudadisi, na watu wazuri kuwadadisi ni hao hao