Skip to main content

Posts

Showing posts with the label maisha mazuri

Bichwa kubwaaa tiny brain......

Women....sio kwamba tuna mabig head bana ni nywele tu hizo. ...Pia hatuna tiny Ubongo isipokuwa sehemu kubwa ya Ubongo wetu inatumika. Yaani tunatunza mambo mengi sana na hufanya tuwe na kumbukumbu nzuri kuliko wenzetu.... si wajua Data zikikaribia kujaa kwenye PC au Simu which is PC. ...isn't it?.....speed inapungua. Unajikuta unakuwa mvivu kufikiria kwa undani kabla hujasema matokeo yake unatoa lolote halafu unagundua neno likitoka halirudishiki.....unabaki kujuta au ku justify. Wanaume ambao walikaribia wanawake ni wale waliotumia 1/3 ya Ubongo wao na baadhi yao ni JK Nyerere, Gandhi na B Mkapa(no Nkapa really I just liked him as prezzo). Kama hutaki kuamini nikuambiacho kuhusu matumizi yetu ya Ubongo nenda kaGUGE. (Googling......kaguge usisahsu you heard it here 1st). Binafsi huwa nafikiria huku naongea au kuandika na matokeo yake huwa si justfy bali nasimamia nilichokisema na kukusaidia kunielewa. So wacha uvivu, soma magazeti ambayo ni broadsheet sio tabloids. ...wacha bl

Kabla hujafa, hujaumbika!

Ni kawaida ya watu (wengi) kucheka matatizo ya wenzao au kuyazungumzia katika mtindo wa "kichekesho". Mimi napenda sana kucheka na kuchekesha (japo kuwa sichekeshi....yaani nikitoa kichekesho watu hawacheki mpaka nielezee kwanini nilichosema kinachekesha)....hihihihi achana na hili! Matatizo nayogusia hapa ni yale ambayo mtu hana uwezo wa kuyazuia, sio matatizo ya kujitakia(kuchagua) kama vile Utumiaji wa Madawa (japokuwa hata hawa mie huwa siwacheki). Kama huna utu na huna mpango wa kumsaidia mwenye matatizo kwanini uzungumzie matatizo yake kwa watu wengine katika hali ya "kumcheka"? Wengine wanapoleta habari za mtu za kusikitisha kutokana na matatizo yake yaliyobadilisha Mwili au Akili (Ulemavu) yake hawacheki kwa kukenua Meno, lakini jinsi wanavyoelezea unagundua kabisa wanamcheka mhusika. Mf; "Eh bwana unamkumbuka Elia? Daah jamaa yaani kaisha halafu sasa anatembelea Mgongo. Yule jamaa alikuwa anajifanya mjanja sana"....umeona? Hakenui meno laki