Skip to main content

Make up artists....

Ukiingia kwenye Department stores au Boots (Duka la Dawa na Vipodozi) kubwa kwa sie wa Ulaya hii hapa....unakutana na MUA kwenye "viOSK" vyao wenyewe wamejiremba wamependeza....er kwa mbali!




Asa sinilikuambia tangu nigonge miaka 30....sasa ni 30na nimeanza "kuipenda" ngozi yangu ya usoni! "Mambo ya mwanamke reception".....sasa kama mtu hukujaaliwa "reception" nzuri au kurembeka(mimi) basi angalau Ngozi iwe nzuri na yenye afya kuwapotezea watu "focus".




Mwanamke nimejaribu bidhaa kibawoo za kufanya Uso wangu uwe laini na wenye rangi moja....maana...mmh!




Sijawahi kutumia Mkorogo (na sina mpango huo), sina tatizo na Chunusi (mpaka nile Chocolate), yaani ngozi yangu inakaribia ukawaida tu japo inatoa mafuta ya kutosha kukaangia Vitumbua....anyway!




Nimejaribu skin care nilizokuwa nikitumia miaka ya nyuma in my late 20s, sasa zinadunda, kitu cha uso ama kimekomaa au kimekuwa Sungu (Kisayansi ngozi hupoteza nini sijui nini na nini...so yeah)!




Si ndio nikaenda kwenye moja ya kiOsk ili kununua Bidhaa hiyo (baada ya kutumia Sample kwa Wiki mbili) inayoifaa ngozi yangu yenye Mafuta "ya kukaangia"....Samaki!





Baada ya hapo nikapewa na darasa la Make up kutoka same brand (sio Mac Dar combine by the way).....sasa MUA mtoa darasa anaisifia bidhaa na kusema hata yeye anaitumia na leo "kaivaa"....namwangalia Usoni naona imemvaa yeye!





Hata sijui kwanini nakuambia haya! Hata hivyo ile Serum niliyoinunua imeifanya ngozi yangu ya Uso kuwa even....hivyo basi nitarudi nikainunue ingine hii ikiisha japo ni ghali....aah! nawekeza kwenye Ngozi ya Uso, huwezi jua huko Mbeleni naweza nikawa Supa Modo Kizee wa kwanza wa Kitanzania Nchini hapa......(najicheka hapa balaa)



Babai.
Mapendo tele kwako...

Comments

Topic hizi tamba...

Weusi wa Kwapa na Vipele Makalioni....

Well Weupe huwa hawawi na weusi kwapani bali Unjano au Ukahawia....wale wenye nywele nyeusi sasa ni another case. Kuhusu Vipele makalioni havina Ubaguzi, raha ya vipele vile ni kwamba havionekani kwa Macho....utajua unavyo kwa kujipapasa, au gusa ngozi yako....inakuwa kama ina "mikwaruzo" wajua ile nanihii ya kupiga Msasa mbao? Yep ndio feels kama hivyo! Usione haya sio Ugonjwa na wala sio Tatizo kiafya, ni mambo ya Urembo tu na yawapata watu mbali mbali Ulimwenguni.....kama urembo sio issue kwako basi baki na Mapele yako na uyafurahie! Mimi nilikuwa nayo na siyapendi na ndio maana nataka nikupe mbinu ya "mapambano" ili uwage na Makalio "smooth"....Sasa hapa nikuambie kuhusu Vipele Makalioni au weusi wa Kwapa?.....Yote? Hamna shida twende in to them*. Vipele: Sijui inasababishwa na nini(sio mtaalam mie) ila nahisi ni kutoijali ngozi ya sehemu hiyo ndio inachangia....huisugui ukioga, huilainishi kwa mafuta, unavaa chupi za Mpira badala ya Pamba, huifanyishi

Kuachisha mtoto Kunyonya!

Heeeeeelp!!! Ka Binti kangu kana Mwaka na Nusu (Miezi18) lakini kamo tu, hata dalili ya kuacha hakana....Mie nimechoka kunyonyesha, nimechoka kuwa Mkubwa hapa Chini ya Kidevu bana! Babuu aliacha mwenyewe ghafla, yaani siku hiyo kaamka tu akagoma kunyonya....Mwanamke bembeleza, lazimisha mtoto wapi!!....alikuwa na Mwaka Moja na Mwezi(Miezi 13) na niliteseka Kihisia na Kimwili kwa Wiki nzima. Kihisia: Haina Uzungu hii, ila nililia sana....kwanini Mwanangu hataki kuwa karibu na mimi? (maana kunyonya kwake kulikuwa kunanipa ukaribu na Mwanangu). Nilipanga kumnyonyesha mpaka Mwaka na nusu (Miezi 18), kwanini Kanigaya(Susa) kabla sijawa tayari?!!! Kimwili: Matiti yanauma bwana asikuambie Mutu! Yalivimba(Jaa maziwa)....the more nakamua ndio yanajaa zaidi.....kamata simu Pigia Mama, Mama akasema "usiyakamue kwani ukikamua mwili wako unahisi mtoto anataka kunyonya zaidi so yanajitengeneza kwa Kasi ya ajabu". Kaongeza: "

Mashoga/Wasenge "wanatuibia" Waume/Wapenzi wetu....

...kwanza kabisa napenda utambue kuwa hakuna Mtu anaweza kumuiba  mwenzake kimapenzi, Mpenzi wako anapotoka kwako na kwenda kwa mwingine ni wazi kwamba kaamua kufanya hivyo, hilo sio kosa lako na wala hujasababisha yeye kwenda huko kwingine bali ni yeye mwenyewe na akili zake timamu kafanya uamuzi huo. Tangu Ushoga ndio khabari/Suala Muhimu wacha na mimi nidaivu ini nipate "trafiki" japo nimechelewa. Tofauti na "platform" nyingine hapa utajifunza kwa kiasi kidogo...au niseme kiasi fulani. Linapokuja suala la Ushoga/Usenge,sehemu kubwa ya Jamii imetawaliwa na  Uoga ambao unapelekea kutokuelewa Ushoga ni nini? Hali hiyo ni Asilia, kwamba mtu anazaliwa hivyo au ni uamuzi  wa mtu au ni Hali inayojitokeza ukubwani baada ya Kubalehe.....pale kijana anapoanza kutambua ujisia wake(je anavutiwa/penda Wanawake au Wanaume au wale wa Jinsi kama yake). Mie sio Mtaalam wa Masuala ya Kisenge/Shoga lakini ni mtu ambae napenda kudadisi, na watu wazuri kuwadadisi ni hao hao