Skip to main content

Marafiki(best) ni Milele, Wapenzi waja na kuondoka....

....kweli kabisa (kama upo chini ya miaka 29). Unapofikia umri mkubwa mambo mengi yanabadilika na unajikuta kuwa huitaji Marafiki ili kuwa na furaha(kufurahia Maisha yako). Sio hivyo tu pia unakua/badilika(nao pia) na hivyo mnakuwa hamuendani tena kama ilivyokuwa enzi zile, Matokeo yake unakuwa unafahamiana na watu na sio kurafikiana nao(best friends eeh Siwezi!).





Marafiki wanakusaidia kujifunza kuhusu Maisha (kihisia), wanakusaidia kujua namna ya kukabiliana na Drama za "maisha", wanakusaidia kujua  nini cha kudharau/kushikilia Bango, wanakusaidia kujua kuwa wewe upo tofauti nao, wanakusaidia kujuana nini cha kuchangia/kutokuchangia, wanakusaidia kujua ni wakati gani unatakiwa kuachana na jambo na kusonga mbele, wanakusaidia kuelewa jambo/somo Darasani (tunauelewa tofauti) n.k.





Hivyo ni Muhimu sana tena sana kwa Mtoto kutengeneza Marafiki ili aweze kujifunza hayo niliyoyataja hapo juu. Sio kila kitu Mtoto anajifunza kutoka kwa Wazazi, mengine anajifunza akiwa Shuleni lakini Nje ya Darasa au Michezoni anapokuwa na watu wa umri wake(si Baba na Mama/Walimu).





Mwanao pengine ana"marafiki" wengi na baadhi anawaita mabesti, baadhi yao wananakuudhi  na nisingependa arafikiane nao, lakini unajua kuwa ni muhimu kwake kuwa nao na kuwa na hisia za "u-best friend" ili ajifunze. lakini yeye kuwa na Marafiki hao sio sababu ya wewe kurafikiana na Wazazi wa hao marafiki zake.



Utasema najikanganya(contradict) hapa kwa sababu mie ni Anti-Marafiki, nilishawahi kusema hapa kuwa sina marafiki(sio anti-marafiki) na sidhani kama kuwa na Marafiki ni Muhimu, halafu can be too expensive/stress you out ujue....siku za kuzaliwa, Ndoa, Ubatizo, Chrismas,kutembeleana.....aiii i love my own company....Nafahamiana na watu, sijengi urafiki/sirafikiani nao.




Nilipojifungua HV(Healthy Visitor) akajakunitembelea, akanambia kuwa inabidi nijiunge na "Mother & Baby groups" ili nitengeneze Marafiki wanaoendana na mimi (wazazi wezangu wenye watoto wa umri wa Mwanangu), maana "mabadiliko ya Homono na Kichanga vinaweza kukufanya uwe mpweke sana"....vere vere attempting ila.....



...nkapiga mahisabati: Kukesha+Kunyonyesha+Kuogesha+Kubadilisha+Kupika+Kufua+Kunyoosha(piga pasi)+ Mimi kula(yeah it is a job)+Kusafisha nyumba+Kwenda "mother & Baby"= Sina Energy.


Naheshimu na kuthamini Muda wako hapa, Ahsante kwa Kuichagua Blog hii,
Babai

Comments

Topic hizi tamba...

Weusi wa Kwapa na Vipele Makalioni....

Well Weupe huwa hawawi na weusi kwapani bali Unjano au Ukahawia....wale wenye nywele nyeusi sasa ni another case. Kuhusu Vipele makalioni havina Ubaguzi, raha ya vipele vile ni kwamba havionekani kwa Macho....utajua unavyo kwa kujipapasa, au gusa ngozi yako....inakuwa kama ina "mikwaruzo" wajua ile nanihii ya kupiga Msasa mbao? Yep ndio feels kama hivyo! Usione haya sio Ugonjwa na wala sio Tatizo kiafya, ni mambo ya Urembo tu na yawapata watu mbali mbali Ulimwenguni.....kama urembo sio issue kwako basi baki na Mapele yako na uyafurahie! Mimi nilikuwa nayo na siyapendi na ndio maana nataka nikupe mbinu ya "mapambano" ili uwage na Makalio "smooth"....Sasa hapa nikuambie kuhusu Vipele Makalioni au weusi wa Kwapa?.....Yote? Hamna shida twende in to them*. Vipele: Sijui inasababishwa na nini(sio mtaalam mie) ila nahisi ni kutoijali ngozi ya sehemu hiyo ndio inachangia....huisugui ukioga, huilainishi kwa mafuta, unavaa chupi za Mpira badala ya Pamba, huifanyishi

Kuachisha mtoto Kunyonya!

Heeeeeelp!!! Ka Binti kangu kana Mwaka na Nusu (Miezi18) lakini kamo tu, hata dalili ya kuacha hakana....Mie nimechoka kunyonyesha, nimechoka kuwa Mkubwa hapa Chini ya Kidevu bana! Babuu aliacha mwenyewe ghafla, yaani siku hiyo kaamka tu akagoma kunyonya....Mwanamke bembeleza, lazimisha mtoto wapi!!....alikuwa na Mwaka Moja na Mwezi(Miezi 13) na niliteseka Kihisia na Kimwili kwa Wiki nzima. Kihisia: Haina Uzungu hii, ila nililia sana....kwanini Mwanangu hataki kuwa karibu na mimi? (maana kunyonya kwake kulikuwa kunanipa ukaribu na Mwanangu). Nilipanga kumnyonyesha mpaka Mwaka na nusu (Miezi 18), kwanini Kanigaya(Susa) kabla sijawa tayari?!!! Kimwili: Matiti yanauma bwana asikuambie Mutu! Yalivimba(Jaa maziwa)....the more nakamua ndio yanajaa zaidi.....kamata simu Pigia Mama, Mama akasema "usiyakamue kwani ukikamua mwili wako unahisi mtoto anataka kunyonya zaidi so yanajitengeneza kwa Kasi ya ajabu". Kaongeza: "

Mashoga/Wasenge "wanatuibia" Waume/Wapenzi wetu....

...kwanza kabisa napenda utambue kuwa hakuna Mtu anaweza kumuiba  mwenzake kimapenzi, Mpenzi wako anapotoka kwako na kwenda kwa mwingine ni wazi kwamba kaamua kufanya hivyo, hilo sio kosa lako na wala hujasababisha yeye kwenda huko kwingine bali ni yeye mwenyewe na akili zake timamu kafanya uamuzi huo. Tangu Ushoga ndio khabari/Suala Muhimu wacha na mimi nidaivu ini nipate "trafiki" japo nimechelewa. Tofauti na "platform" nyingine hapa utajifunza kwa kiasi kidogo...au niseme kiasi fulani. Linapokuja suala la Ushoga/Usenge,sehemu kubwa ya Jamii imetawaliwa na  Uoga ambao unapelekea kutokuelewa Ushoga ni nini? Hali hiyo ni Asilia, kwamba mtu anazaliwa hivyo au ni uamuzi  wa mtu au ni Hali inayojitokeza ukubwani baada ya Kubalehe.....pale kijana anapoanza kutambua ujisia wake(je anavutiwa/penda Wanawake au Wanaume au wale wa Jinsi kama yake). Mie sio Mtaalam wa Masuala ya Kisenge/Shoga lakini ni mtu ambae napenda kudadisi, na watu wazuri kuwadadisi ni hao hao