Skip to main content

Posts

Showing posts with the label kids

Marafiki(best) ni Milele, Wapenzi waja na kuondoka....

....kweli kabisa (kama upo chini ya miaka 29). Unapofikia umri mkubwa mambo mengi yanabadilika na unajikuta kuwa huitaji Marafiki ili kuwa na furaha(kufurahia Maisha yako). Sio hivyo tu pia unakua/badilika(nao pia) na hivyo mnakuwa hamuendani tena kama ilivyokuwa enzi zile, Matokeo yake unakuwa unafahamiana na watu na sio kurafikiana nao(best friends eeh Siwezi!). Marafiki wanakusaidia kujifunza kuhusu Maisha (kihisia), wanakusaidia kujua namna ya kukabiliana na Drama za "maisha", wanakusaidia kujua  nini cha kudharau/kushikilia Bango, wanakusaidia kujua kuwa wewe upo tofauti nao, wanakusaidia kujuana nini cha kuchangia/kutokuchangia, wanakusaidia kujua ni wakati gani unatakiwa kuachana na jambo na kusonga mbele, wanakusaidia kuelewa jambo/somo Darasani (tunauelewa tofauti) n.k. Hivyo ni Muhimu sana tena sana kwa Mtoto kutengeneza Marafiki ili aweze kujifunza hayo niliyoyataja hapo juu. Sio kila kitu Mtoto anajifunza kutoka kwa Wazazi, mengine anajifunza akiwa S