...halafu inatumika ovyo sana mpaka imeanza kupoteza Maana kwa Kiswahili(hatuna "like" au hatutaki kutumia kupendezwa) na kwa Kiinglishi. Mtu humjui...ndio kwanza mmekutana, baada ya kubadilishana Salamu, mnaagana na kuambiana "nakupenda".....wengine mnakutana tu anakuambia "Jamani Dada nakupenda". Hujambo lakini? Pia kuna wale Ndugu...."nawapenda kweli wanangu(yaani wanao)"...akiishi nao masaa 24 lazma abadili usemi wake(au hisia zake). Pamoja na kusem ahivyo bado Uzito wa neno Nakupenda upo palepale....mtu akikuambia hivyo lazima karoho karuke kwa Mshangao au kwa Uoga(kama mna-date)....Kama nilivyoahidi kutoka Post iliyopita (bofya hapa ) leo tukumbushane namna tofauti ya kusema "nakupenda" bila kusema neno hilo. Umewahi kuambiwa nakupenda na Mke/Mume wako ukaangua Kicheko halafu unajiuliza Kasoma Blog gani leo? hihihihihi au ni Mimi tu!! sio kwamba neno hilo linachekesha bali huwa hulisikii kutoka kwake. Wapo ambao hu...