Ruka hadi kwenye maudhui makuu

Kama Mke, Umejitosheleza?

Kila Mwanamke ni Imara hiyo inajilikana na wala huitaji kujitanganza(kuwa chini ya Kundi fulani kuthibitisha hilo), pamoja nakusema hivyo  wewe kama Mke bado ni Dhaifu/laini(Kimwili) na hakuna kosa mkimama kuwa mlaini(jivunie  udhaifu wako).


Kazi yako kubwa Duniani ni kuwa msaidizi wa Mumeo, kuleta uhai(kubeba Mimba na Kuzaa), kulea, kufundisha na kutunza Familia.Ili uweze kufanya hayo(niliyoyatajabhapo juu) unatakiwa kuwa  umejitolesha kwenye nyanja nyingine ili kurahisisha Maisha yako kama Wewe, Mama na Mke. Unapaswa kuwa na uwezo  wa kufanya baadhi ya vitu haraka na kwa ukamilifu bila uwepo wa mtu wa pili iwe Mumeo au Muuza Huduma.Je ni nyanja gani hizo?

Dharura; Unaweza kujituliza, kutafakari kwa haraka na kufanya uamuzi kwa faida yako na familia badala ya kusubiri mpaka Mumeo apokee Simu/arudi.


Uchumi; kuwa na Akiba ya Senti kwa mahitaji madogo madogo(ya ghafla) nje ya Bajeti ya Familia(kutoka kwenye zile anazokupa Mumeo), sio kila akikupa Pesa unatumia zote kwa wakati mmoja. 


Elimu; Uwezo wa kuwafunza watoto wako na kuwasaidia wanapokwama Kimasomo, ili kukuza uelewa wao wa Somo husika wanapokwenda Shule.


Nyumba; Usafi wa Mazingira...kuibadili Nyumba na kuwa Nyumbani kwa kila mtu sio familia yako tu. Uwezo/juzi wa kurekebisha mf; bulb imeungua au "fuse" imekata  sio mpaka uite Fundi Umeme/usubiri Mumeo akuje.


Tendo; Unahamu, badala ya kulianzisha, unasubiri mpaka Mumeo akusogelee? Acha hizo.


Labda leo mwendo ni mrefu, badala ya kulalamika, kuonyesha haupo "interested" na kubaki umelala kama gogo...kuwa na mbinu (sio kukata kiuno)za kumfanya awahi "kucheka" na wakati huo huo wewe kufurahia safari.


Kujijali/Jipamba; Jifunze kutengeneza Nywele, Kucha, kujiremba n.k ikitokea Salon zimefungwa *cough* Covid19  Lockdown *cough*.


Na mwisho kabisa, Jifunze aina tofauti za Mapishi, aina 3 za kushona/repair nguo(hasa kama una watoto).


Je, wewe ni Mke uliejitosheleza? Ongeza zako basi na mie niongezee kwangu.


Muda wako unathamani kubwa kwangu, ahsante. 
Bai.

Maoni

Zile Maarufu

Kuachisha mtoto Kunyonya!

Heeeeeelp!!! Ka Binti kangu kana Mwaka na Nusu (Miezi18) lakini kamo tu, hata dalili ya kuacha hakana....Mie nimechoka kunyonyesha, nimechoka kuwa Mkubwa hapa Chini ya Kidevu bana! Babuu aliacha mwenyewe ghafla, yaani siku hiyo kaamka tu akagoma kunyonya....Mwanamke bembeleza, lazimisha mtoto wapi!!....alikuwa na Mwaka Moja na Mwezi(Miezi 13) na niliteseka Kihisia na Kimwili kwa Wiki nzima. Kihisia: Haina Uzungu hii, ila nililia sana....kwanini Mwanangu hataki kuwa karibu na mimi? (maana kunyonya kwake kulikuwa kunanipa ukaribu na Mwanangu). Nilipanga kumnyonyesha mpaka Mwaka na nusu (Miezi 18), kwanini Kanigaya(Susa) kabla sijawa tayari?!!! Kimwili: Matiti yanauma bwana asikuambie Mutu! Yalivimba(Jaa maziwa)....the more nakamua ndio yanajaa zaidi.....kamata simu Pigia Mama, Mama akasema "usiyakamue kwani ukikamua mwili wako unahisi mtoto anataka kunyonya zaidi so yanajitengeneza kwa Kasi ya ajabu". Kaongeza: "

Weusi wa Kwapa na Vipele Makalioni....

Well Weupe huwa hawawi na weusi kwapani bali Unjano au Ukahawia....wale wenye nywele nyeusi sasa ni another case. Kuhusu Vipele makalioni havina Ubaguzi, raha ya vipele vile ni kwamba havionekani kwa Macho....utajua unavyo kwa kujipapasa, au gusa ngozi yako....inakuwa kama ina "mikwaruzo" wajua ile nanihii ya kupiga Msasa mbao? Yep ndio feels kama hivyo! Usione haya sio Ugonjwa na wala sio Tatizo kiafya, ni mambo ya Urembo tu na yawapata watu mbali mbali Ulimwenguni.....kama urembo sio issue kwako basi baki na Mapele yako na uyafurahie! Mimi nilikuwa nayo na siyapendi na ndio maana nataka nikupe mbinu ya "mapambano" ili uwage na Makalio "smooth"....Sasa hapa nikuambie kuhusu Vipele Makalioni au weusi wa Kwapa?.....Yote? Hamna shida twende in to them*. Vipele: Sijui inasababishwa na nini(sio mtaalam mie) ila nahisi ni kutoijali ngozi ya sehemu hiyo ndio inachangia....huisugui ukioga, huilainishi kwa mafuta, unavaa chupi za Mpira badala ya Pamba, huifanyishi

Mashoga/Wasenge "wanatuibia" Waume/Wapenzi wetu....

...kwanza kabisa napenda utambue kuwa hakuna Mtu anaweza kumuiba  mwenzake kimapenzi, Mpenzi wako anapotoka kwako na kwenda kwa mwingine ni wazi kwamba kaamua kufanya hivyo, hilo sio kosa lako na wala hujasababisha yeye kwenda huko kwingine bali ni yeye mwenyewe na akili zake timamu kafanya uamuzi huo. Tangu Ushoga ndio khabari/Suala Muhimu wacha na mimi nidaivu ini nipate "trafiki" japo nimechelewa. Tofauti na "platform" nyingine hapa utajifunza kwa kiasi kidogo...au niseme kiasi fulani. Linapokuja suala la Ushoga/Usenge,sehemu kubwa ya Jamii imetawaliwa na  Uoga ambao unapelekea kutokuelewa Ushoga ni nini? Hali hiyo ni Asilia, kwamba mtu anazaliwa hivyo au ni uamuzi  wa mtu au ni Hali inayojitokeza ukubwani baada ya Kubalehe.....pale kijana anapoanza kutambua ujisia wake(je anavutiwa/penda Wanawake au Wanaume au wale wa Jinsi kama yake). Mie sio Mtaalam wa Masuala ya Kisenge/Shoga lakini ni mtu ambae napenda kudadisi, na watu wazuri kuwadadisi ni hao hao