Skip to main content

Posts

Showing posts with the label bongoceleb

Weusi wa Ngozi sio Uchafu....

....ila usipokuwa muangalifu kwenye kuchagua Rangi za Mavazi/Nywele hakika utaonekana Mchafu(huvutii), hii  haina kujiamini.....nadhani ni muhimu kuchagua Rangi zinazoendana na Rangi ya Ngozi  yako. Mambo?!! Kuna siku nipo na mishughuliko yangu ya ndani wakati Asali wa Moyo anatazama Mashindano ya Tenesi ya Wibledoni. Anapendezwa sana na wale Williams Dadaz....mmoja wao alikuwa anacheza. Mwenyewe anafurahia uchezaji wake (au kuona Tako  kila kisketi chake kinapoinuka hihihihi maana mdada mMashallah). Sina hili wala lile nasikia mwenznagu anawasifia wadada Williams kwa kutokuwa kama Celebs wengine.....mie nkasema hao sio ma-Celeb ni Sports Stars (kwa Kiswahili ndio tunasemaje vile?) ila Media inalazimisha kuwaweka kwenye Kundi la M-aceleb kitu ambacho sio haki kwasababu wapo walipo kutokana na kazi/kujituma kwaoo na sio kuonekana kwenye Tv au kuuza Haidthi kwenye magazeti au....oh well kwa Umalaya. Katika kufunga maelezo yangu nikamalizia na....kiukweli mie siwaelewi

The Online Support....kwa Celebs!

Hata kwa sie ambao sio maCeleb is real.....unajua pale unapoungwa mkono na kupewa ushirikiano wa "kisaiba"(cyber) na kukufanya ujihisi umebebwa....unapendwa...unakubalika. Unahisi furaha na pengine kujiona Mashuhuri(mtu wa kawaida) au kuhisi Umashuhuri wako (kwako Celeb) umeongezeka na kupata Konfisensi ya ajabu ya kufanya lolote au chochote. Unajua ile umeweka Picha halafu unapata followers zaidi na wanakumwagia masifa.....wanaomba kuona zaidi na wewe unazimwaga picha za mapozi tafauti hihihihihi baada ya siku mbili wanakuja followers wapya(wale wale kwa account tofauti via device tofauti) na kuanza kukuponda.....unabaki kulia na kuita watu "fake friends". Inategemea ni nini hasa kimefanya upate support ya "Fanzi" aka followers wako Online.....kuna wakati unahisi kutaka kusema ukweli wako ulivyo na sio uongo wausikiao au ku-justfy na ku-share zaidi ya unachopaswa kusema/ku-share. Bila kuomba ushauri kutoka kwa "inner self" au bila kumsikili