Habari yako?
Nilikuwa Likizo ya Kiangazi.....katika hali halisi nilipaswa kukujulisha lakini nikahisi kama vile nitakuwa najionyesha au napitiliza ku-share so nikapiga kimya. Anyway habari kwa ufup, kama bado unajali ni kwamba Madoa ya Tetekuwanga(Chickenpox) yamepungua Weusi.
Ujisedhani hali ya Hewa ya UK inafanya Ngozi kutakata haraka ndugu, nilipewa Mkorogo(andikiwa dawa ya kuondoa Weusi) nitumie kwa Muda wa Wiki 8. Baada ya kugusa Wiki ya Pili nikaona Vijitundu vya ngozi(pores) vinapanuka! Aiiii nikautupilia mbali Mkorogo.
Duania ya leo inamengi na kila kukicha tunaongezewa sheria za namna ya Kuishi vizuri au kuishi na watu kwenye jamii. Tunaambiwa tusiwajaji wenzetu kitu ambacho sio rahisi kwa sababu kujaji ni asili ya mwanadamu, pia bila kujaji hakika utakuwa unafanya maamuzi mambovu na hivyo kuishi ukilalama "kwanini mimi".
Nimekwishawahi kukuambia hapa(kwenye blog hii) kuwa mie huwa najaji watu/mtu kama wewe ila tofauti yangu mimi na wewe(hello hihihihi) ni kuwa, huwa najitahidi kuelewa na kukubali kwanini wapo walivyo au kwanini wanafanya wafanyavyo nikishindwa naishia na "but why?". Sina tabia ya kumchukia mtu au kumcheka ama kumdharau kwasababu nimepitisha "jajimenti" kutokana na muonekano wake au matendo yake mabaya ya awali ama Ugonjwa/matatizo yake kiafya.
Nina uhakika kabisa sio Mimi tu ambae najaji watu ama vitu na pengine vitendo vya mtu kabla sijamjua/fahamu......naamini wewe pia unajaji kabla hujafanya uamuzi wa Kurafikiana na mtu au kununua Kiwanja au nyumba na pengine Bidhaa fulani kwa ajaili ya matumizi binafsi au ya familia.
Sasa unaposhupaa kuwaambia wenzio kuwa "msinijaji mpaka mnijue kwanza" unakosea.....kwasababu hakuna mtu ana muda wa kusubiri akujue kwanza halafu apitishe "jajimenti".....mfano mdogo ni pale Mabinti wanapogombania kuwa ma-Miss, pamoja na vigezo vinavyowekwa bado unakuwa "judged" na Jamii kabla hawajapata nafasi ya kukujua(via magazeti ya Udaku).
Nukta ni kwamba usiogope kujaji kwasababu ni "human nature" wakati mwingine huwezi kujizuia kwasababu kuna poster zinasema "dont judge me before you know me" sijui "nenda kafanye kazi badala ya kunijaji".....wakati unajaji unakuwa njiani kwenda Job.
Babai.
Comments