Kwa sie Wafanyakazi huwa ni kawaida kushindia khanga/Pjs mwisho wa Wiki kwasababu tunatilia kila siku tuendapo kazini. Lakini je ikitokea umeamua kuwa Mama wa nyumbani kwa Muda(mie) utakuwa upo hivyo siku zote Saba za Wiki kwa Muda wote Mpaka mtoto aanze Shule?. Ni rahisi sana kujisahau na kupoteza "utambulisho" pale unapokuwa una-deal na watoto muda wote. Unafubaa, na ikiwa Nguo zako nyingi zilikuwa Office like ndio kabisaa(nani anavaa kiofisi wakati yupo nyumbani?).
Skinny Jeans nazo ni shughuli....!
Hapo ndio kutafuta Ari kunajitokeza....ni vema kuwa/kupata/kupewa Ari(kuwa Ispired that is) kwa uHasi ama uChanya.....zote ni hisia na ukizipata pengine unaweza kuzitumia kufikisha ujumbe kwa watu wengine au ukaepuka na labda kujifunza kama sio kupata nafuu kuwa "aah am not the only one then".
Mfano: Kuna Binti mmoja Maarufu ambae Kijamii anaonekana kuwa na Mwenendo mchafu na ni Mfano mbaya kwa Mabinti wengine ambao wanakuwa "ispayadi" na mambo ya kishenzi afanyayo. Binti huyo alitajwa kuwa ni Mmoja kati ya Wananawake wanaowapa Ari mabinti wengine. Sasa wengi(mie mmoja wapo) waliona sio sahihi kwa Mtu mwenye tabia chafu kutoa Ari kwa watu wengine(hasa wadogo).....lakini tulisahau kuwa Ari inaweza kuwa Hasi au Chanya in which zote ni muhimu(hukua unalodhani litakusaidia, mengine mwachie mwenyewe).
Mtu huwezi kumtegemea mtu mwingine(sababu tu ni Kioo cha Jamii) ajibebe utakavyo wewe ili tu wanao wasijekuharibikiwa, wanao kuharibikiwa haina uhusiano na mtu mwingine bali wewe kama Mzazi na wao wenyewe kama wao. Achana na hili!
Nakumbuka enzi natwiti kuna watu walikuwa wanakerwa na watu wanaoleta Habari za Instagram, badhi walikuwa wakisema kama umekerwa au kufurahishwa sasa si ukamalizie huko huko Insta, kwanini unatuletea sisi huku kwenye Platifomu ingine? Hawa nao hawakujua/hawajui kuwa kule ni "chanzo" kama ilivyo Twitter/Facebook kwenye Taarifa ya Habari.
Anyway, mie sio Fashionista wala Stylist na sina "style".....well nilidhani-aga Staili yangu ni "Casual chic/Smart" kumbe nlikuwa najiongopea.....hata hivyo napenda kupendeza/kuvaa vizuri lakini sifuati TRENDY. Sasa wakati wa Mimba halafu tena nikawa STHM(stay at home mum) nikajikuta mimi na Leggings(abarikiwe aliebuni hizi makitu) tunauhusiano mzuri.
Kibibi alipoacha kunyonya na mie nikaanza kulala bila kusumbuliwa n ahivyo kuanza kufurahia Maisha(hehehehe) nkasema, nahitaji kuwa na style(ambayo bado sina), sasa natakiwa kufanya nini ili kuwa Stylish Mum of 2 in her 30s going on 40s?(ningekuwa stylish ninge-blog)....this time nilihitaji kusikia na kuona na sio kusoma hivyo nika-Ytube.
Hakukuwa na 30s wala 40s.....wengi ni 40+(as in 50 mapaka 200? sijui),Curvy/Plus Size(hawa ni wengi hadi wanakera hihihihi fat peeps).....wakati nakaribia kukata tamaa nikakutana na Busbee Style Bonyeza hapa . Pata Ari ili ujue wapi pa kuanzia.
Naheshimu na kuthamini Muda wako hapa, ahsante kwa kuichagua Blogg hii
Babai.
Comments