Skip to main content

Posts

Showing posts with the label stylish

Kipindi cha Baridi ndio unahisi kuwa Stylish....

Jambo! Nimeamua kuipenda Autum/Winter sasa, sio tu kuwa Kipindi hiki ndio najihisi kuwa stailishi bali pia napata nafasi ya kutumia(vaa) kila aina ya nguo niliyonayo kwa Kujiamini zaidi kwasababu hakuna  ile "presha" ya Kunyoa Kwapa wala Miguu na Mikono.....(well naficha chini ya Tights, Jaketi au Koti). Halafu Majira haya ni Marefu kuliko hizo siku 3 za Kiangazi. September Mpaka June ni total Baridi. mekosa Pic ya Mweusi ambae ana-stayle kama yangu (ubaguzi kando) Halafu pia Wivu wa hali ya hewa unakuwa hauumi sana kwa walio  Nchi za joto, unajua kuna muda unaangalia Fashinblogs za Tz halafu unapata Wivu wa hali ya hewa.....wanavalia nguo nyepesi na wanafurahia Kiangazi kwa Muda mrefu zaidi yako. Kipindi cha Kiangazi huku kinadumu kwa Mwezi mmoja, tena sio Mwezi Mzima mnapata Jua la maana bali mara mbili au tatu kwa Wiki ndani ya Miezi 3! Sasa kuna ulazima gani ya kuipenda Summer(Kiangazi)? Halafu huku tulikohamia Mwaka huu Kiangazi kilijitokeza kwa Si

Mama wa Nyumbani kujipenda/pendeza.....Nani anakupa Ari?

Kwa sie Wafanyakazi huwa ni kawaida kushindia khanga/Pjs mwisho wa Wiki kwasababu tunatilia kila siku tuendapo kazini. Lakini je ikitokea umeamua kuwa Mama wa nyumbani kwa Muda(mie) utakuwa upo hivyo siku zote Saba za Wiki kwa Muda wote Mpaka mtoto aanze Shule?. Ni rahisi sana kujisahau na kupoteza "utambulisho" pale unapokuwa una-deal na watoto muda wote. Unafubaa, na ikiwa Nguo zako nyingi zilikuwa Office like ndio kabisaa(nani anavaa kiofisi wakati yupo nyumbani?). Skinny Jeans nazo ni shughuli....! Hapo ndio kutafuta Ari kunajitokeza....ni vema kuwa/kupata/kupewa Ari(kuwa Ispired that is) kwa uHasi ama uChanya.....zote ni hisia na ukizipata pengine unaweza kuzitumia kufikisha ujumbe kwa watu wengine au ukaepuka na labda kujifunza kama sio kupata nafuu kuwa "aah am  not the only one then". Mfano: Kuna Binti mmoja Maarufu ambae Kijamii anaonekana kuwa na Mwenendo mchafu na ni Mfano mbaya kwa Mabinti wengine ambao wanakuwa "ispayadi