Kumbuka sababu kuu ya ninyi kuwa pamoja ni mapenzi na sababu ya kufunga Ndoa ni kwavile mnapendana na mnataka kuishi pamoja kwa furaha. Ulipenda na ukataka kupendwa na kufurahia Muungano wenu. Sasa kama hiyo ndio sababu kuu, kuna umuhimu gani wa kuendelea kuishi Maisha ya ndoa wakati hakuna furaha? Utasema Mapenzi, kwasababu mapenzi hayaishi obviously, jinsi mnavyozidi kuishi pamoja ndivyo ambavyo unapata sababu nyingine nyingi kwanini unapenda Mume/Mkeo.
Kuna wakati
unaweza usipendezwe na mumeo/mkeo kutokana na matendo yake au kutokana na jinsi
alivyokujibu/ongea nawe au kafanya jambo Fulani hukubaliani nalo, hii hali
hutoweka mara akiomba radhi au wewe ukiamua kudharau. Hali hiyo haiondoi
mapenzi yako kwa mume/mkeo.
Ule msemo wa watu wa social media kuwa “my happiness comes first” au “I choose me” ni kwa wale ambao hawana Imani (hawamuogopi Mungu) ni single au wapo kwenye Ndoa mbaya za unyanyaswaji, vipigo, mateso na masimamngo. Sie wengine ambao wenza wetu wamebadilika sababu zilizo nje ya uwezo wetu Mf; wamezaa au kupoteza kazi/mali n.k. "your family’s happiness comes first” au tuseme “furaha ya mkeo/mumeo comes first”, yeye akiwa na furaha, wewe pia utakuwa na furaha na hivyo watoto yenu kufaidika pia.
Sasa kabla
sijakukumbusha namna ya kurudisha furaha kwenye ndoa yako(ambayo siijui), sio mbaya kama
tukiangalia ni vitu gani hasa vinachangia kuondoa furaha kwenye Ndoa yenu?
1-Mmesahau au hamzingatii zile nguzo 5 zisome hapa , hapa na hapa kwasababu mmemzoea kupita kiasi na sasa upo tu hapo kutimiza wajibu, mmejisahau.
2-Unamtolea
nje/unamkataa Mumeo kimwili na hii ikitokea mumeo anakosa furaha napengine kuanza
kuwaza wapi unapata tendo ama hakuvutii tena au anakasoro(inategemea na kiwango
cha kujiamini kwake). Kwa kifupi Mumeo ni sensitive sana kwenye kutolewa nje kimapenzi. Yanayoendelea akilini mwake hupelekea kujitenga kihisia(anakununia),
akikununia wewe unanuna back au unaanza kulalamika na matokeo yake mnazozana na
mwishowe kutamkiana maneno makali au kurudisha makosa ya zamani yaliyokwisha
tatuliwa(malizwa).
3-Wakati
wote upo tayari kujitetea au ku-react, ku-over-react ni kubaya sana mara zote unaachia akili yako kwenda mbali na kutengeneza “hadithi” ili kupata majibu kwanini mkeo/mumeo
kauliza alichouliza, kasema alichosema n.k. Pia wakati mwingine unaweza kuwa unafanya kitu ambacho unajia wazi kabisa mkeo/mumeo akiona ataudhika na hivyo unaweka Ngao tayari kupambana(kujitetea).
4-Kupeana triggers
kila kukicha, kila mmoja wetu anazo ni vema ukiziweka wazi ili mwenza wako azifahamu na hivyo kuziepuka ili usiwe triggered…kuanzia Ex, baadhi ya Marafiki zake, kutoka
home bila kuaga, matumizi ya pesa, malezi ya watoto, kurudi nyumbani usiku wa manane n.k.
5-Umesahau kufanya yale ambayo ulikuwa unayafanya awali mlipokuwa wapenzi, wachumba na Ndoa ilipokuwa changa. Mf, wewe Mume ulikuwa unampigia simu Mkeo na mnaongea masaa yote unapokuwa break kazini, ukiwa safari hulali mpaka usikie sauti yake, ukitoka unambusu kwa mahaba na unamjulia hali kati kati ya siku na kabla ya kurudi nyumbani unamjulisha.
Habari zako na zake ndio muhimu na sio Habari za Dunia au Siasa. Mlikuwa mnazungumzia Mipango yenu ya baadae, careers, safari n.k. Mlikuwa mnafanya mapenzi kila siku(siku hizi mnafanya ngono tu), mnaenda kulala pamoja na hata kama mmekosana hamlali bila kupeana busu nyevu la usiku mwema(na kuishia kufanya mapenzi kwa hasira?), unakumbuka?
Njoo tena ili tuone hatua unatakiwa kuchukua ili kurudisha furaha kwenye Ndoa yenu.
Bai!
Comments