Skip to main content

Mti/Ua Shamba....

Yenye viwango na Uchunguzi wake umefanywa kisasa.....(Wataalam wa Sayansi) sio wale wa "Maono"....The wezi.




Oh! Heri ya Juma Nne....Hongera na ahsante kwa kuichagua Blog hii.



Ile Nywele issue (bado ninayo) bana inanifanya nijifunze mengi kuhusiana na vitu asilia ambavyo vinamanufaa mazuri kwa mwili wa Binadamu ikiwa ni pamoja na nywele.




Kunywa maji ni muhimu kwa ajili ya ngozi, nywele na kupunguza Mafuta Mwilini kwani inakuzuia kula chakula kingi/kupita kiasi.....ila ukiwa ulibeba mtu mbili Tumboni eh bwana lazima uwe mwangalifu na maji unywayo.





Unakunywa "Fundo" ndogo mbili na sio kumimina robo/nusu Lita kwa wakati mmoja....unaeza pata Mimba atifisho a.k.a Kitambi....(Hata sijui kwanini nakuambia hili)!




Oooh! Back to Miti shamba, ninayotaka kuizungumzia hapa ni Chai.....huyoo ulidhani mizizi na Magome? Hehehehe....Chai ya Kijani na ile ya Maua aina ya Chamomile.



Come to think of it, Mizizi na Magome hutumiwa kama Chai pia eti?...."chemsha kisha Unywe/Oga", anyway....




Asali wa Moyo wangu anatabia ya kuninunulia Chai za aina mbali-mbali asa siku moja akaja na "Chamomile Tea"....bila kujua nkatengeneza na kuweka Sukari....aiiii manukato na radha yake ikanishinda.





Mara Chai zote za kusaidia ku-relax zikaisha ikabaki "Chamomile" na "Green Tea"(inaradha ka' dawa)....nikajitutumua na kuanza kuinywa "Chamo", sasa bila sukari....ikanyweka vema.





Nikaendelea nayo kila jioni, ndani ya Wiki 3 nkaaza kuona Nywele zinaanza kujaa pale mbele(hair line).....aiii mwanamke nkaenda Google+Wikipedia=Ukweli wa Mti/Ua shamba husika......Mimi na "Chamomile Tea" pamoja Milele.





Leo hii Mimi na Asali wa Moyo tunaadhimisha Miaka Kadhaa ya Muungano wetu.....kama na wewe unaadhimisha basi Happy Anniversary to ya! .


Babai....
Mapendo tele kwako...

Comments

Topic hizi tamba...

Weusi wa Kwapa na Vipele Makalioni....

Well Weupe huwa hawawi na weusi kwapani bali Unjano au Ukahawia....wale wenye nywele nyeusi sasa ni another case. Kuhusu Vipele makalioni havina Ubaguzi, raha ya vipele vile ni kwamba havionekani kwa Macho....utajua unavyo kwa kujipapasa, au gusa ngozi yako....inakuwa kama ina "mikwaruzo" wajua ile nanihii ya kupiga Msasa mbao? Yep ndio feels kama hivyo! Usione haya sio Ugonjwa na wala sio Tatizo kiafya, ni mambo ya Urembo tu na yawapata watu mbali mbali Ulimwenguni.....kama urembo sio issue kwako basi baki na Mapele yako na uyafurahie! Mimi nilikuwa nayo na siyapendi na ndio maana nataka nikupe mbinu ya "mapambano" ili uwage na Makalio "smooth"....Sasa hapa nikuambie kuhusu Vipele Makalioni au weusi wa Kwapa?.....Yote? Hamna shida twende in to them*. Vipele: Sijui inasababishwa na nini(sio mtaalam mie) ila nahisi ni kutoijali ngozi ya sehemu hiyo ndio inachangia....huisugui ukioga, huilainishi kwa mafuta, unavaa chupi za Mpira badala ya Pamba, huifanyishi

Kuachisha mtoto Kunyonya!

Heeeeeelp!!! Ka Binti kangu kana Mwaka na Nusu (Miezi18) lakini kamo tu, hata dalili ya kuacha hakana....Mie nimechoka kunyonyesha, nimechoka kuwa Mkubwa hapa Chini ya Kidevu bana! Babuu aliacha mwenyewe ghafla, yaani siku hiyo kaamka tu akagoma kunyonya....Mwanamke bembeleza, lazimisha mtoto wapi!!....alikuwa na Mwaka Moja na Mwezi(Miezi 13) na niliteseka Kihisia na Kimwili kwa Wiki nzima. Kihisia: Haina Uzungu hii, ila nililia sana....kwanini Mwanangu hataki kuwa karibu na mimi? (maana kunyonya kwake kulikuwa kunanipa ukaribu na Mwanangu). Nilipanga kumnyonyesha mpaka Mwaka na nusu (Miezi 18), kwanini Kanigaya(Susa) kabla sijawa tayari?!!! Kimwili: Matiti yanauma bwana asikuambie Mutu! Yalivimba(Jaa maziwa)....the more nakamua ndio yanajaa zaidi.....kamata simu Pigia Mama, Mama akasema "usiyakamue kwani ukikamua mwili wako unahisi mtoto anataka kunyonya zaidi so yanajitengeneza kwa Kasi ya ajabu". Kaongeza: "

Mashoga/Wasenge "wanatuibia" Waume/Wapenzi wetu....

...kwanza kabisa napenda utambue kuwa hakuna Mtu anaweza kumuiba  mwenzake kimapenzi, Mpenzi wako anapotoka kwako na kwenda kwa mwingine ni wazi kwamba kaamua kufanya hivyo, hilo sio kosa lako na wala hujasababisha yeye kwenda huko kwingine bali ni yeye mwenyewe na akili zake timamu kafanya uamuzi huo. Tangu Ushoga ndio khabari/Suala Muhimu wacha na mimi nidaivu ini nipate "trafiki" japo nimechelewa. Tofauti na "platform" nyingine hapa utajifunza kwa kiasi kidogo...au niseme kiasi fulani. Linapokuja suala la Ushoga/Usenge,sehemu kubwa ya Jamii imetawaliwa na  Uoga ambao unapelekea kutokuelewa Ushoga ni nini? Hali hiyo ni Asilia, kwamba mtu anazaliwa hivyo au ni uamuzi  wa mtu au ni Hali inayojitokeza ukubwani baada ya Kubalehe.....pale kijana anapoanza kutambua ujisia wake(je anavutiwa/penda Wanawake au Wanaume au wale wa Jinsi kama yake). Mie sio Mtaalam wa Masuala ya Kisenge/Shoga lakini ni mtu ambae napenda kudadisi, na watu wazuri kuwadadisi ni hao hao