Majuzi nilikuwa nakatiza mitaa ya YouTube nikitafuta best Female TV talk show Bongo Tanzania baada ya kukumbuka enzi nikiwa msichana kulikuwa na kipichi cha wanawake, siku mbuki jina wala Host wake ila Jaquline Ntuyabaliwe (sasa Mrs Mengi) alikuwa mshiriki, ilidumu kama episodes 3 hivi(kila Ijumaa/Jumamosi)..unfortunately sikupata nilichokuwa natafuta ila nikakutana na podcast/Youtube Channel ya Salama, nikawa nasikiliza mazungumzo na mgeni wake, which was quite interesting then kwa chini I saw there were kijibango anaomba "kuchangiwa" as in donate to the channel/podcast, I thought these people have no mshipa wa aibu.
Am used to other youtubers asking for money or as they demand "cash Up me:, "donate first ndio nitaanza kuongea", "join my channel for elfu 3(£1) kwa mwezi to get exclusive"...but Dada si Muajiliwa kule Sekta ya private which they pay better than Serikalini...No? au mazungumzo yake na Mastar ni side haso?
Huwa najiuliza, I (you) subscribed to a few youtube channels, say 25 na they all ask for £5 a month depends on how popular they are and their Content quality na juu ya hapo nalipia YouTube premium(I don't) family plan £18 which makes £143, so nikulipe wewe pound 5 per month kwasababu unabwabwaja ubeya wa wasanii, showing your beautiful life style or whatever you do in front of a Microphone baada ku research your ( kuokoteza) info which I can do that myself if I want? No. ila ukute ni wewe na mimi tu ndio we ain't got money so wivu unatusumbua ndio maana hatutaki kulipia memberships.
Sababu ni nini?
Sijui maana mie sio mtaalamu, ila imefika mahali sasa naamini kuwa social media imefanya watu wapoteze haiba na values zao, kwamba ime desensitised watu na hivyo they don't have shame anymore. Sio shame tu hata ile huruma(Utu) ilibaki kiasi hakuna tena. Kuna mtu alisema Social midea imejaa psychopaths au inafunza watu kuwa self-centred na u-psychopath(sio wote wanazaliwa hivyo, sometimes malezi na mzingira yanaweza kukubadilisha/athiri). Maisha yako ya online ni sehemu ya mazingira yako.
Kwanini imekuwa rahisi kwa watu kuomba-omba online?
1-Muibuko wa "influencer as a career" kwamba ukiwa na follower wengi unaeza watumia kujiingizia kipato kwa kuwauzia bidhaa kutoka kwa Kampuni mbali mbali. Ile connection uliyonayo naukaribu"fake" wako na wao unaweza kuwafanya followers kuamini kuwa wanakujua nje-ndani na hivyo kujenga "mahusiano" na wewe via support. Inafikia mahali watu wananunua bidhaa/huduma ili tu waku-support na kuwa karibu nawe. Easy money.
2-Upweke wa Watu wa Ughaibuni; Mtu alie nyumbani anaona anawafuatiliaji wa kipindi au account yake akionyesha kusaidia watu wenye matatizo kiuchumi/maradhi au maish akwa ujumla(unakumbuka how Shogongo alivyoanzaga na gazeti lake la Ujumaa?). Sasa watu elfu kadhaa wamejiunga kwenye Acc, anapiga mahesabu kwamba ikiwa kila mmoja anatoa £3 which is very small amount and anybody wa Ughaibuni can afford, hakika nalipwa mshahara wa Laki kadhaa kwa mwezi.
Kwasabau katika hali halisi YouTube halipi watu kiasi hicho, ukiona watu wanasema YouTube inawalipa na wamekuwa mamilionea, ni wazi kuwa wana direct sponsorship and as you buy what they sell you(from the sponsorship) the sponsor get what they paid for kwa client wao, a YouTube channel you subscribed to.
Sio tu kwenye Kipato kutokana na content creation, siku hizi watu wamekuwa wepesi kuomba senti hasa kutoka kwa wabongo wa Ughaibuni, kila wakipatwa na Gonjwa, Bill ya matibabu, wakifiwa mbio online. Hawa wabongo wa zamani(wamejilipua hehehehe) ambao sasa wanaishi maisha comfortable wanasumbuliwa na upweke, au midlife crisis wanataka kujisikia vema na kuwa karibu na nyumbani kila kuwa wamechangia, si ujajua homesick na hawawezi kurudi nyumbani? Huwa wepesi sana kujitolea kwasabu wanajua ugumu wa Maisha kwa baadhi ya watu Tanzania, wanaamini wakijitolea angalau wanakuwa wamesaidia wenzao kama Sadaka maana mchango wao wa £100(tSh 300k*) is nothing.
Nini kifanyike?
Utamaduni na Mila; kurudi nyuma na kujitahidi kujenga mahusiano mazuri na watu wanaotuzunguuka kwenye jamii, kabla ya internet wazazi wetu(waliozaliwa 1950s/60s) walifanya nini? walichangishana wenyewe kwa wenyewe kwenye familia na koo zao, majirani, mtaani, kazini, Kanisani/Msikitini, shuleni n,k.
Politically yanatakiwa kufanyika Mengi, tukianzia na Mfumo mzima wa Elimu, Ajira, Tax na Afya ili watu wawawe na Elimu, vipato vya uhakika, kuwa na huduma bora za afya na Bima ya Afya bure kwa kila mwananchi ambae hana ajira au ana kipato cha chini.
Kwasababu tu watu wa kwenye internet wanafanya haina maana kuwa hata wewe ufanye, wabongo tuna Mifumo yetu Asilia kwenye kila jamii(depends na Mkoa/Kabila), sio unakaa sana online to the point that you forget who you are, your values, principles and culture. Stop Americanise ya self.
Hitimisho;
Ukute I look at this on a poverty mindset au tuseme eye, maana I guarantee you nina Material nyingi tu za kutengeneza pesa, sema nini sina that confidence to take a step further and asking people for money so we can all be abundant and live our best soft life.😉
Bbai.
Comments