....when Viongozi wote ni umri wako au wadogo kwako,
Unakumbuka May 2, 1997 Tony Blair alikuwa Waziri Mkuu mdogo UK? Alikuwa kundi moja kiumri na Mama yangu ila sawa na Dingi. Hapa nilipo najihisi kama mama alivyojihisi mwaka huo(well I was not her then so I don't really know how she felt).
Awali, binafsi nilihisi nipo nyuma ki-career kwasababu nilichukua time off kulea wanangu badala ya kuachia Childcare industry, sio hivyo tu kufanya kazi halafu mshahara wote unaishia kwa Walezi wa watoto wako ni dhambi. Yaani unabaki masikini halafu wakati huohuo huwajui wanao na wao hawakutambui kwasababu hujawahi kuwalea. Mbaya zaidi wakikua wanakuchukia na kumpenda Miss Amanda, kumsikiliza Mr Cook and kumuheshimu Mrs Mcmun huku wewe ukishangaa na kujiuliza kwani nimekosea wapi? Kwanini tabia haziendani na Values zenu(baba na mama).
Mara pap! Nikakumbuka, Wakati wenzangu akina Macron, Jacinda wa NZ (alikuwa mdogo zaidi ila kazi ilimshida), Sanna Marin wa Ufini, Georgia Meloni wa Italia, Viongozi wa UK (baada ya Boris wote wadogo ila ni wa ovyo ovyo kama maCCM hawastahili heshima ya kutajwa) wanaongoza vyama na nchi, mie nipo busy na-shape vijana wa Taifa lijalo.
Sasa wapo Secondari wananifanya nikumbuke enzi zangu, nafurahi tumefika kwenye umri tunaongea na kujadili topics kama watu wazima, hasa wakati nawafundisha. Kipindi wapo Msingi bana, ilikuwa ngumu sana kuelewana kwasababu technically kielimu nilikuwa mbele as nilisoma Masomo tofauti zaidi ya 7 tangu nipo la 3.šŖ
Unaogopa uzee au umejikubali na kumshukuru Mungu umefikia umri huo na kupata uzoefu wa kuwa "middle aged" maana sio kila mtu anabahati ya kufika hapo ulipo. Pia unapata nafasi ya kukumbuka enzi zako hakukua na stress za social media, overflow of useless information, ukosefu wa ajira, Utapeli wa high wealthy life, soft life, kujiajiri, uuzaji wa Kozi/Maombi ya kuwa tajiri/kupata ajira ambazo hazipatikani, different kind of life style trends oooh bila kusahau possions za kuvutia Wanaume wenye mahela, high value men(not high quality) kutoka South Afrika na Congo and Kozi za Women's health na Pain management kutoka America.
Yaani Dunia imekuwa kijiji, kila mtu anamjua mwezio kiundani na matatizo yake japo wanaishi Mabara 7 tofauti. No wonder Vijana wa leo wadogo zangu wapendwa wana kongoroka haraka, Mwanamke/Mwanaume wa miaka 28 ni kama 54. Terrible.
Anyways, kuwa makini usipotee kiimani halafu baadae uanze kujitafuta na kudhani Mkeo/Mumeo na watoto wenu wamekuchelewesha kufikia Malengo yako so unawaacha ili ukaanze miasha upya somewhere. Si unajua ile trend ya "I come 1st, gotta love myself 1st"....well is not for you who brought other innocent people in your life, Watoto.
Heri ya Mwaka mpya 2024!
Bai.
Comments