Tuesday, 29 May 2018

Dini inaweza kuyumbisha Ndoa/Uhusiano wako....


Heri ya J'Nne,

Kama nilivyokuahidi Wiki (mbili na Siku Moja) iliyopita (bonyeza hapa kama ulipitwa) kuwa nitakuja nikukumbushe tu ni kwa namna gani Imani yako ya Dini inaweza kuyumbisha Ndoa au Uhusiano wako.


Kwa kawaida wengi hudhani kuwa mtu anapokuwa Mumini Mzuri wa Dini au "anamuogopa" Mungu ndio atakuwa muaminifu, atampenda kwa dhati, atakuwa  mkweli, hatomuumiza na mengineyo mazuri mazuri.


Ukweli ni kuwa Mtu wenye Dini mara nyingi huwa mwepesi kutenda "dhambi" au yale ambayo hayaruhusiwi na Dini zao akijua kuwa atasamehewa, sio tu na Mungu bali wewe Mwenza wake unapaswa kumsamehe. "Ikiwa Mungu aliemuumba anatuambia tusamehe iweje wewe ushindwe kunisamehe".


Mazoea hayo ya kutegemea kusamehewa kila unapofanya makosa ya makusudi hupelekea upande mmoja kuhisi upweke na kuondoa Amani na Furaha kwenye Uhusiano /Ndoa. Hii inaweza kupelekea kujitenga na pengine kutafuta furaha Nje ya Muungano wenu. Hilo moja.


Pili, Imani yako ya Dini inakuzuia kufurahia Tendo vilivyo kwa kuwa "Freak" unapokuwa faragha na Mumeo au mnakuwa waoga kujaribu vijimambo vingine ili kufurahia uumbaji wake Mungu. Unahisi kuwa Mungu hatopendezwa kwa sababu wanaofanya hayo ni "Malaya".


Sasa kwa baadhi, wakikosa "u freak" kutoka kwa wenza wao, huamua kujaribu nje....ukimuona Mama wa Mchungaji/Mtumishi anavyojiheshimu huwezi amini anayoyafanya kwa Kiongozi wa Kwaya. Ukimuona Sheikh huwezi kuamini anayofanyiwa Mwalimu wa Madrasa(hihihihihi), kabla hujakasirika, hebu malizia aya ya mwisho.


Nnacho jaribu kusema hapa ni kuwa Imani yako ya Dini isiwe Kikwazo cha wewe kushindwa kumunysha Mwenza wako Ujuzi, Utundu, wehu wako n.k mnapokuwa Faragha. Natambua mmeambiwa maneno yafananayo na  "Mume huna mamlaka juu na Mwili wako bali Mkeo na Mke huna Mamlaka juu ya Mwili wako bali Mumeo"....hii haina  maana kufanya Tendo kwa namna ile ile kila siku, bali kuwa huru kuufanyia chochote (kizuri) Mwili wa mwenza wako ili kumpa Raha(well this is my logic).


Nisikuchoshe, nathamini Muda wako hapa.
Mapka wiki Ijayo....kwasasa, bai!

Monday, 14 May 2018

Social Media, kama ilivyo kwa Dini ni chanzo cha Ndoa/Uhusiano wako kuyumba.


Jambo!

Siku kadhaa niliuliza "kiutani" kuwa Tatizo la Upungufu wa Nguvu za Kiume  kwa Vijana(chini ya Miaka 60)Nchini Tanzania au pengine Afrika linasababishwa na nini? Wawili watatu walidai kuwa Vijana siku hizi wanapiga Mkono(kujichua) kupitiliza, binafsi nilidhani kuwa ni Mawazo kutokana na Ukosefu wa Ajira(Kipato).


Hivi majuzi nikakutana na Majadiliano ya Vijana (huku niliko) wakijadili ni namna gani Instagram inawafanya washindwe kuwa watendaji wazuri Kitandani. Sio tu kwamba hawawezi ku-perform bali pia wakifanikiwa kuinuka basi mwenzo huwa mreeeefu na hawafikii mwisho.


Kwa kawaida(kiuzoefu) Mzunguuko wa kwanza unaenda kwa Dakika 45 bila Mwanamke kuhisi kuchoka na bila kubadilisha Mikao(unabadili movements za Kiuno/Nyonga), na hii ni kwa Mwanamke mwenye uwezo wa "kukojoa" zaidi ya  mara moja ndani ya Mzunguuko Mmoja(Hisabati nazo zinanifuata kila mahali...I don't like them huh!).


Kumbuka baada ya Mwanamke(wa kawaida, sio sie special wa Goli 3 per Mzunguuko hihihihi) kufika Kileleni(kukojoa) ataweza kukusindikiza kwa dk nyingine 20, zaidi ya hapo anaishiwa "hamu" na kuanza kukauka na hivyo kufanya Tendo kuwa karaha.


Sasa unajiuliza Insta inaingilianaje na Mwendo mrefu au kushindwa kiutendaji? Well ni rahisi tu. Mwanamke wako sio kama wale unaowaona kwenye Instagram. Huenda wewe ni mmoja kati ya wale wengi ambao Mlifunga Ndoa kwa kufuata Tabia njema/Alikuwa mbele yako/Umetafutiwa/Umri unakutupa Mkono na sio Tabia njema, Mwonekano uutako kipindi chote kabla ya Uzee na labda Akili na utayari wa kutulia(umemaliza Starehe za Ujana).


Nani anafanya mapenzi na Akili au Tabia njema? Sawa  pengine kwenu Wanaume muhimu ni kuingiza tu basi, lakini kuwa wazi na nafsi yako! Utataka kuingiza tu ikiwa huna jinsi (upo desperate) lakini ukiwa na Choice/option sidhani kama utaingiza tu popote, lazima macho yako yapendezwe, yavutike na muonekano wake.


Au kama hujaoa basi inakuuwia vigumu kuwa na Mwanamke umtakae kama wale uwaonao Instagram. Mara nyingi unatamani ungefanya nao mapenzi, lakini kutokana na umbali au viwango inakua ngumu. Lakini kwasababu ni Insta inakuwa rahisi kwako kumfuatilia/wafuatilia wachache wanaokuvutia na hata kuzungumza nao.


Ikiwa unatumia muda Mwingi na Insta(Twita na platform zingine) THOTs/Models au Wake za watu inaweza kuathiri Utendaji wako na ukajikuta unahitaji Pombe kali kama vile Jack Daniels au Konyagi, pengine Viagra za Kiasili ili kufanya Tendo vilivyo. Unaweza kudhani ni kawaida yako kupiga Pombe Kali.....lakini ukweli ni kuwa huwezi tena Kiasili kwasababu Picha uliyonayo Kichwani inayokuvutia sio huyo Kimama aliekitandani/mbele yako. Umekuwa tegemezi wa Pombe/na Dawa.


Matumzi ya Bidhaa hizo hukufanya uende mwendo mrefu kupita Kiasi, Mf Jack Daniels unaweza kuondoka hata Masaa Matatu(Kwa Wanawake ukuje next time nikuambie jinsi ya kukabiliana na mwendo mrefu huku ukifurahia) na bado usifikie Mshindo.


Hapa Mwanamke anajishtukia na kudhani kuwa hakuvutii tena kwasababu siku hizi hauji haraka kama zamani, yaani madoidoe yake yote yanapita bureee hata lile Bao la kwanza  baada ya Siku tatu bila Tendo linachukua Nusu saa kuja. Anaanza kukuhisi vibaya, anahoji, analaumu n.k.


Wewe (Mwanaume) pia unaweza kudhani kuwa Mpenzi wako hakuridhishi tena na hajui, kajisahau au unaanza kupoteza Uanaume wako na hivyo kujaribu mwingine nje ya Uhusiano uone tofauti....yeah kuna mijamaa mijinga that much. Badala ya kutafuta suluhu na kubadilisha inaenda kuongeza tatizo. Na huo ndio mwamnzo wa kuyumba kwa Ndoa/Uhusiano wako.


Dini inayumbisha Ndoa/Uhusiano? weeee! Usikose Wiki ijayo.

Kwasasa tambua kwamba nathamini Muda wako hapa na Shukrani kwa Ushirikiano.

Babai.

Monday, 7 May 2018

Jinsi ya kukabiliana na Mwanaume apendae kununa/susa/chuna...Sio kwamba anapenda (hakuna mtu anapenda kununa)isipokuwa anatabia ya kununa(Kislani/Gubu). Kama ilivyo kwa sisi Wanawake, wenzetu pia huwa wananua ila kununa huko huwa wanakupa Jina lingine tofauti kabisa na Kisilani/Gubu ili wasihusishwe na "Uanamke"(wakiamini ni udhaifu na Mwanadamu pekee dhaifu Akilini mwao ni Sisi).


Utamsikia anang'aka na kusema hana gubu/hajanuna/hajajitenga isipokuwa "siku yangu imeharibika/imeanza vibaya", "usinisumbue nina Mawazo", "Nahitaji muda wa peke yangu kutuliza akili", "Najisikia vibaya" na ikiwa alipoteza Mzazi au Wazazi wote basi hiyo itatumika zaidi..."nimewakumbuka Wazee" nakadhalika.


Tabia hiyo inakera na inaumiza sana, inakupa wewe Mke mtu upweke wa hali ya juu. Inaweza kukupa ushawishi kwa ku-check na Ex au hata kutamani kutafuta kipoozeo. Hivyo kusababisha mtikisiko kwenye Ndoa/Uhusiano wenu ikiwa hakuna Mawasiliano au hamjuani(hamjasomana tabia, kwamba bado ni Wapenzi wapya).


Mara nyingi Mwanamke anaweza kudhani  labda humpendi/jali tena, huenda kuna mtu Mpya(unatoka nje ya uhusiano) au unataka kuachana nae na hivyo unatafuta sababu.


Upweke na Maumivu kwako huongezeka pale unapogundua kuwa anazungumza na Rafiki zake  na kuchekelea(onyesha anafuraha) au Watoto wenu tu lakini wewe unapata majibu ya "Ndio" na "Hapana" na Sura ya Kisilani, au wakati wa kutoka hakuagi kama kawaida yake(sisi ni Busu halafu "am off", ninyi ni nini?)....basi unapata "Am off" tena akiwa Mlangoni....ili usiisikie then akirudi umsute(lalamike) vizuri.Wakati wa kufundwa(tuliofundwa Oyee)tulifunzwa kuwa Mume anapofanya hivyo(kununa) huwa anatafuta mahali pa kutolea  yaliyoujaza Moyo wake, Wanaume wengi sio wepesi wa kuongelea "hisia" zao . Hivyo wanaamua kukununia ili ukasirike halafu mzozane na hapo apate kuyatoa mahisia yake na ionekane chanzo ni wewe wakati ni yeye.


Muhimu ni kuhakikisha yupo salama lakini muache na kununa kwake mpaka awe tayari ku-share na wewe(in 3 days max). Bila kukupotezea muda na kuongeza urefu wa Bandiko hili, nikuambie ni namna gani unaweza kukabiliana na hilo na hivyo kuepusha Ugomvi;-


Ukigundua "siku yake imeanza vibaya"(ana Gubu/Kanuna/Kajitenga hihihihi), tafuta sababu ya yeye kuwa alivyo leo na muulize kwa upendo tatizo ni nini? Jibu atakalo kupa lichukue, liheshimu na umuache alivyo. Usibishe wala kuongeza ya kwako na hivyo kumuudhi. Hilo moja.


Pili; Endelea na shughuli zako za kila Siku kama kawaida, onyesha kumjali ila usipitilize.

Tatu; Pamoja na kuwa ni ngumu kushirikiana nae Kimwili, jitahidi kumpa atakapohitaji(hasa cha asubuhi).

Nne; Ikiwa wewe ni kama mimi, kwamba unapika kama sehemu ya kuonyesha Mapenzi na umpendae kakununia unaweza kutaka kususa kumpikia ili umkomeshe. Usifanye hivyo, pamoja na ugumu wake kihisia wewe Mpikie  chakula akipendacho.

Tano; Kila mnapoenda kulala, mpe kumbatio(kumhakikishia kuwa unamjali sio la kutaka Tendo).

Sita; Kama mnaishi pamoja Kununa Mwisho siku Tatu, kama mpo mbali mbali mwisho Wiki. baada ya  muda huo lianzishe ili aache kununa. Usianze kwa kulalamika, isipokuwa mkumbushe umuhimu wa kuwasiliana na kuchangia matatizo ya kihisia/kiakili. Kama Wenza ni muhimu kuweka wazi issues na kuzitatua pamoja.

Atafunguka na kuomba radhi na kujielezea. Hakika utashangaa kwanini sasa asingekuambia tangu Siku ya kwanza ulipomuuliza tatizo ni nini? Kumbuka wewe na yeye ni watu wawili tofauti, sio kijinsia tu bali Malezi, Mazingira mliokulia, pengine Kabila/taifa, uwezo kiakili/kimaamuzi, ujasiri n.k.


Nathamini Muda wako, karibu hapa usome Faida za Kununa kwa Mwanamke.

Kwa leo Baibai.