Heri ya mwaka Mpya! Sasa umegonga zaidi ya 40 unajisikiaje? Nakumbuka nilipokuwa in my 20s Ma-Celeb walikuwa wanasema wanajisikia kama walivyokuwa in their 20s....wakaibua msemo wa 40s in new 20s. Kwangu binanafsi nakuhakikishia sio kweli kwa asilimia Mia moja, kwasababu nilipokuwa na umri nusu wa nilionao sasa, sikuwa najiamini kwenye kufanya maamuzi Kiuchumi, Kimwili na Kimahusiano(ndugu, marafiki, mpenzi) na kijamii kwa ujumla. Kama ulichelewa kuwa na watoto basi ujue utapoteza umuhimu wa baadhi ya mahusiano na watu wengine sababu watoto wako ni muhimu zaidi kwa sasa kuliko hao watu wengine, sio hivyo tu wanao wanakupa sense ya ukamilifu na kuridhika na maisha uliyonayo na hutaki kupoteza muda kufanya mambo nje ya familia yako ulioitengeneza na Mumeo/Mkeo. Kwa wale waliokuwa na watoto ktk umri mdogo, wanaweza kuikuta wapweke sababu watoto wamekua na wanajitegemea hivyo ktk umri wa miaka 40na unaweza kujikuta unatamani kujenga mahusiano na watu wengine nje ya Mwenza wako ...