Skip to main content

Posts

Showing posts with the label kupendwa

Kama Mumeo anakupenda hatoruhusu ufanye haya...

Kutokana na wakati tuliopo ambapo  kuna "informations" nyingi kuhusu nini hasa Mwanamke anapaswa kufanya au kuwa na hivyo kuibua kukanganyana na kudanganyana kuliko wakati wowote ule wa maisha ya Mwanadamu(nimeongeza chumvi, sijui historia ya Mwanamke kabla ya 1900). Hata hivyo bado haiondoi  ukweli kuwa kuwa Mwanamke  mbele ya Wanawake wa kisasa ni Kazi ya Ziada. Mara nyingi sie(wewe na wenzio) wa Kisasa huwa tunaambiana kuwa mwanaume hana haki juu ya mwili wako au uamuzi wako wa nini unataka kufanya na mwili wako(mavazi/Urembo) which it is true  kama ni Mpitaji(boyfriend) lakini ukiwa  kwenye Ndoa/Uhusiano Mwanaume kuonyesha kuwa anajali nini unaweka juu ya mwili wako ni dalili kuwa mwanaume huyo anakupenda na sio kwamba hajiamini au anahofua kuibiwa. Wengi mnadanganyana kuwa Mume(au Mume mtarajiwa) akikukataza usifanye mambo kadhaa ni kuwa anaku-control, Nyanyasa au ni Dikteta kwenye uhusiano wenu. Tunasahau kuwa yeye ni mwanaume na hivyo anajua ni namna gani Wana

How to(Jinsi ya)...kuwa Chini ya "Mumeo"....

....imekuwa kawaida kwa Wanandoa Wake kwa Wame kutafuta "jinsi ya" kufanya mambo mbali mbali ili kuifanya Ndoa kusimama Imara na kuepusha misuko-suko ya kihisia na hivyo kupelekea Ndoa kuwa Ndoano na pengine kuharibika. Hii kuwa "chini ya Mumeo" hata mie siijui na vyovyote ilivyo kamwe sitokubali kuwa "Chini" ya  Mtu yeyote achilia mbali Mwanaume ila nitakuambia ninachokijua ambacho huenda ni tofauti lakini bado kinamrudishia Mwanaume hali ya kujihisi/sikia kuwa anaheshimika/heshimiwa na Mkwe. Tatizo kubwa linalofanya Wanawake kukumbushwa au lazimishwa na Jamii kuwa ni LAZIMA wawe chini ya Wanaume (asiwe na Sauti) pale wanapoamua kufunga Ndoa ni kutokana na Imani kuwa Mwanamke anaposimama na "kujitetea" na/au kum-challenge Mwanaume basi huesabika kuwa hana Adabu, hana Heshima kwa Mwanaume husika. Ukweli ni kuwa unapokuwa kwenye Ndoa ya "ndio Bwana"  kwamba kila anachokisema Mwanaume wewe unakubali tu....huondoa Changamoto