Skip to main content

Posts

Showing posts with the label kuthaminiwa

How to(Jinsi ya)...kuwa Chini ya "Mumeo"....

....imekuwa kawaida kwa Wanandoa Wake kwa Wame kutafuta "jinsi ya" kufanya mambo mbali mbali ili kuifanya Ndoa kusimama Imara na kuepusha misuko-suko ya kihisia na hivyo kupelekea Ndoa kuwa Ndoano na pengine kuharibika. Hii kuwa "chini ya Mumeo" hata mie siijui na vyovyote ilivyo kamwe sitokubali kuwa "Chini" ya  Mtu yeyote achilia mbali Mwanaume ila nitakuambia ninachokijua ambacho huenda ni tofauti lakini bado kinamrudishia Mwanaume hali ya kujihisi/sikia kuwa anaheshimika/heshimiwa na Mkwe. Tatizo kubwa linalofanya Wanawake kukumbushwa au lazimishwa na Jamii kuwa ni LAZIMA wawe chini ya Wanaume (asiwe na Sauti) pale wanapoamua kufunga Ndoa ni kutokana na Imani kuwa Mwanamke anaposimama na "kujitetea" na/au kum-challenge Mwanaume basi huesabika kuwa hana Adabu, hana Heshima kwa Mwanaume husika. Ukweli ni kuwa unapokuwa kwenye Ndoa ya "ndio Bwana"  kwamba kila anachokisema Mwanaume wewe unakubali tu....huondoa Changamoto