Skip to main content

Posts

Showing posts with the label kuwaujifunze

Juice na Soda husababisha "Homa" zisizoisha kwa Watoto....

Heri ya Mwezi mpya wa May. Mungu abariki kila jema upangalo kufanya(na-sound kama Pastor sasa eti?)! Umewahi kujiuliza kwanini Mwanao/Wanao huwa na Homa au Vikohozi visivyokwisha? Ukimpeleka Hospitali na kupima Damu na kila kitu majibu ni kuwa hana Malaria wala Typhoid (hatuna huku ila inawezekana ulipo haya Magonjwa yapo) na magonjwa Mengine ya Utotoni. Wahenga...well Bibi yangu alisema "Mwanangu kuwa Uyaone", mie nasema kuwa na Watoto ujifunze! Wazazi wengi huamini kuwa Soda  husababisha  Watoto kuchangamka kupita kiasi na pengine kukosa usingizi, baadhi huamini kuwa hufanya Watoto kuwa na tabia za ajabu(wabishi,wakahidi, hawakusikilizi, wananguvu kupita kiasi) kutokana na Soda ambayo huwafanya kuwa "high". Sasa hizo ni Soda na zina some sort of "hewa" sio, kwamaana hivyo Juice za kawaida ambazo hazina Sukari ni salama(nilidhani) tena zile ambazo unachanganya na Maji(squash) ndio Bora zaidi(nilijidanganya). Kuna wakati tulikuwa tukinunua