Kutokana na wakati tuliopo ambapo kuna "informations" nyingi kuhusu nini hasa Mwanamke anapaswa kufanya au kuwa na hivyo kuibua kukanganyana na kudanganyana kuliko wakati wowote ule wa maisha ya Mwanadamu(nimeongeza chumvi, sijui historia ya Mwanamke kabla ya 1900). Hata hivyo bado haiondoi ukweli kuwa kuwa Mwanamke mbele ya Wanawake wa kisasa ni Kazi ya Ziada. Mara nyingi sie(wewe na wenzio) wa Kisasa huwa tunaambiana kuwa mwanaume hana haki juu ya mwili wako au uamuzi wako wa nini unataka kufanya na mwili wako(mavazi/Urembo) which it is true kama ni Mpitaji(boyfriend) lakini ukiwa kwenye Ndoa/Uhusiano Mwanaume kuonyesha kuwa anajali nini unaweka juu ya mwili wako ni dalili kuwa mwanaume huyo anakupenda na sio kwamba hajiamini au anahofua kuibiwa. Wengi mnadanganyana kuwa Mume(au Mume mtarajiwa) akikukataza usifanye mambo kadhaa ni kuwa anaku-control, Nyanyasa au ni Dikteta kwenye uhusiano wenu. Tunasahau kuwa yeye ni mwanaume na hivyo anajua ni namna gani Wana