Skip to main content

Posts

Showing posts with the label penzi

Nguzo 5 za Mahusiano...Heshima kwa Mumeo.

Nilikuacha solemba eti, natumai upo salama,..mie mzima kabisa ahsante kwa kujali. Bila shaka unewahi kuona/soma/sikia watu wakisema "Mwanaume haitaji kupendwa bali kuheshiniwa", kwamba Heshima kwake ndio kupendwa...lies the Internet tells. Mwanaume anahitaji vyote, Heshima na kupendwa....ila ukifikiria kiundani(inategemea na situation iliyokufanya ushushe heshima kwake ) kumpenda Mume wako bila kumheshimu ni ngumu. Acha kufikiria kiundani. Pengine Mumeo amewahi kukuambia kuwa anahisi kuwa huna heshima kwake...halafu ukang'aka na kudai sio kweli, kwamba mbona unamheshimu sana tu! Heshima kwa Mwanaume(Mumeo) ni tofauti na vile unamuacha anajiachia kwenye Internet/Bar na wadada wengine, kutopinga maamuzi yake hata kama ni mabaya/hatarishi, kutokuvaa mavazi fulani n.k. Hivi ndio unavyopaswa kumheshimu Mumeo ukiachilia mbali kumsikiliza pia usizungumzie mapungufu yake kwa watu wengine hata kama ni Mama yako. Thamini Ndoa yenu (sio kuishi kwa mazoea) na ikitoke mmepishana na ku