Skip to main content

Posts

Showing posts with the label typhod

Sijafa-sijaumbika....

Si nikaumwa Tetekuwanga!!! Isije siku tunakutana ukaanza kunifokea/Suta kwanini nilisema nina ngozi nzuri wakati nimejawa na madoa ka Chui(as if unajali). So wacha nijihami mapemaa. Sikutegemea kuwa siku moja ningeugua Ugonjwa huu so nilipoanza kuumwa nkasema Mimba nini? Unajua....unapofanya Mapenzi nyama kwa nyama na Mumeo kitu cha kwanza kuangalia ni Mimba kila unapojisikia vibaya ili nisijetumia Madawa nakuua au kulemaza Kiumbe(sio kwamba naitaka hiyo Mimba). Ndio hivyo sasa nimeugua gonjwa la Kiwahili(sio kweli).....akati nakua kuna watu (Majirani zetu) walikuwa wanatukuza magonjwa ya Kudumu kama vile Moyo,Kisukari nakadhalika. Utasikia "sie hatuumwi magonjwa ya Kiswahili kama Tetekuwanga, Typhod, Kifua kikuu na mengine yote ya kuambukiza. Tunaumwa Magonjwa ya maana kama vile Kisukari, Saratani, BP" hihihihihi.....sijui ulikuwa utoto wao au ujinga wao? Sitoki nje bila kujipaka tope(foundation) kuficha Madoa Meusi usoni....naaa hakuna kujiamini hapa.....natisha hahah