Skip to main content

Posts

Showing posts with the label uchaguziUK

Tuepushie Bunge la Kuheng'i....

...na tuepushie huyu wa sasa....amen!  Natumai Kura yangu itaongeza palipopungua 2010. Heyaaa! Kuna wiki moja huwa inakuwa busy sana na appointments kuliko.....Dentist....Chanjo kwa Kibibi....kuongezea Chanjo kwa Babuu....manunuzi ya viwalo vyao vya summer. Wengine (mimi) tunanunua nguo Sikukuu to sikukuu. Unafanya kubadilisha Makoti na Majaketi ya Miaka 2 iliyopita.....sio kila Majira ya mwaka yanavyobadilika mweee. Halafu mtu anakuambia "hutaki kuzaa kwasababu unaogopa maisha".....no dear naogopa gharama. Well ukiachilia habari ya kukujulisha kwanini sijapost kwa muda kiasi, ni kwamba huu uchaguzi wa Leo unanipa Presha kimtindo. Naenda kulala ili niweze kufuatilia matokeo kuanzia saa Tatu(Tano tz). Ahsante kwa kuichagua blog hii. Babai.

Kiswahili Kigumu....spesho Post kwako!

Heyaaa. Ahsante kwa kuichagua Blog hii. Naona Idadi inaogezeka kila siku. Hi wa USA...How do you do wa hapa nilipo....jambo Afrika Mashariki.....Hello wengine wote popote mlipo Ughaibuni. Tambua kuwa ninathamini ugeni na ukazi wako wa muda mfupi au mrefu(unaposoma).....natumaini naweka makunyazi usoni kwako ama kwa kutabasamu au kwa kukunja sura. Umewahi kuamishwa(na Gugo) kutoka Kiinglishi kwenda Kiswahili halafu ukashindwa kuelewa....yaani unachanganyikiwa na hujui nini kina maanisha nini? Kwasababu ninablog kwa Kiswahili mara nyingi Gugo wananijaribu kutumia Blogger kwa Kiswahili ambayo siielewi. Mara chache nasoma Blog za Kiswahili kama vile http//www.tech255.com , www.bwaya.blogspot.com (simu haniruhusu kuweka link so yeah copy and paste uone waandikacho)na nyingine za Kuelimisha. Huko pia huwa nachanganyikiwa na kutokuelewa baadhi ya maneno ambayo nadhani ni mapya. Ila tofauti ni kuwa yapo kwenye sentensi hivyo inanirahisishia kuelewa Mwandishi alimaanisha au anamaanisha n