Heri ya mwaka Mpya! Sasa umegonga zaidi ya 40 unajisikiaje? Nakumbuka nilipokuwa in my 20s Ma-Celeb walikuwa wanasema wanajisikia kama walivyokuwa in their 20s....wakaibua msemo wa 40s in new 20s. Kwangu binanafsi nakuhakikishia sio kweli kwa asilimia Mia moja, kwasababu nilipokuwa na umri nusu wa nilionao sasa, sikuwa najiamini kwenye kufanya maamuzi Kiuchumi, Kimwili na Kimahusiano(ndugu, marafiki, mpenzi) na kijamii kwa ujumla. Kama ulichelewa kuwa na watoto basi ujue utapoteza umuhimu wa baadhi ya mahusiano na watu wengine sababu watoto wako ni muhimu zaidi kwa sasa kuliko hao watu wengine, sio hivyo tu wanao wanakupa sense ya ukamilifu na kuridhika na maisha uliyonayo na hutaki kupoteza muda kufanya mambo nje ya familia yako ulioitengeneza na Mumeo/Mkeo. Kwa wale waliokuwa na watoto ktk umri mdogo, wanaweza kuikuta wapweke sababu watoto wamekua na wanajitegemea hivyo ktk umri wa miaka 40na unaweza kujikuta unatamani kujenga mahusiano na watu wengine nje ya Mwenza wako ...
....vipi kuhusu Elimu, Dini na Familia? Aah Elimu ni kwa ajili ya masikini kwani haina faida, sababu watoto wa vigogo wanainunua. But tunahitaji wajuzi wa afya ya Ubongo, Mwili na viungo vyake, Mifupa n.k kuanzia tupo tumboni mpaka tunafika miaka 120(yep tunafika huko as hii ni karne ya 21 sio 11). Wajuzi wa mazingira,vyakula, sumu, Madawa, Nishati, Shetia na utaratibu wa kulinda na kupata Haki yako maka mtendwa au mtendewa jambo kinyume cha sheria n.k. Vipi kuhusu Imani ya Dini? Nayo tumeaminishwa tu na Wazungu na Waarabu ili watutawale si ndio? Vipi Waarabu na Wazungu huko makwao ambao bado wanafuata, kuamini na kusimamia Imani hizo za Dini, wanafanya hayo ili kujitawala? Aaah ili kunyanyasa Wanawake na watoto....Achana na Uislamu/Ukristo, vipi Imani za Dini/Miungu ya kimila na Desturi? Bado unaamini haikuwa sehemu nzuri ya kuifanya jamii husika kuwa na structure na hivyo kufanya maisha yawe rahisi kumudu hasa linpokuja suala la stress, shida na matukio mengine ambay...