Wazazi wengi wanalea watoto wao kimagharibi bila kuishi Magharibi kwasababu Umagharibi unavutia au ni kwasababu inakufanya ujione bora, tofauti au upo juu zaidi ya wenzako ambao wanalea watoto wao kibongo-bongo ndani ya Tanzania?
Usijisikie vibaya sababu hata mimi nalea wanangu kibongo-bongo wakati hawajahi kuishi Bongo kwa zaidi ya miezi kadhaa ndani ya miaka yote ya umri wao.
Humu ndani hatuwezi kutumia "kumbuka ulikotoka" au "usisahau nyumbani" sababu nyumbani kwao ni England na ndio walikotoka na walipo....Sasa unafanyaje kuhakikisha wanao wanakuwa kibongo-bongo as well as ki-kwao(walipozaliwa)?
1: Hakikisha wanapata values na principals ulizokuwa nazo kama mbogo. Unafanikisha hili kwa kuwapa simulizi za ukweli kuyokana na uzoefu wako wa Mila na Desturi, pia kutokana na uzoefu wako wa huko mlipo na unavyoijua Kacha hiyo hakikisha una-up date inapohitajika. Mf:-
Bongo: Heshimu wakubwa wako. Ngambo: Heshimu anaekuheshimu bila kujali umri. n.k.
2-Vyakula, hakikisha unapika vyakula asilia vya kibongo-bongo na vile vya Kimila na Desturi, usisahau kuwahusisha kwenye mapishi.
3-Balehe, kwa mtoto wa kike hakikisha inakuwa sherehe kama ulivyofanyiwa wewe japo itakuwa wewe mama na yeye Binti yako, hakikisha siku hiyo inakuwa special....kikwetu, hii siku ni special sababu wanataka usione Hedhi kama mzigo au kitu kibaya so unapewa zawadi, wanawake wote wanakusanyika na kufurahi pamoja, wanakupa tips za kukabiliana na Hedhi unakaa ndani kwa siku saba na kurelax, ku-enjoy zawadi zako na kula utakacho specially made for you.
Hii itabaki nae maisha yake yote ya Hedhi. Hii ni kwa wa mjini so kuna vitu waliacha as havikuwa na umuhimu kwa Binti wa Mjini ambae her goals haikuwa Kuolewa ktk umri mdogo.
4-Mipaka: Hakikisha unaiweka mapema na inaheshimiwa...as watoto wanakua wanaanza kukuona wewe kama mwanamke/mwanaume kwanza halafu ndio Mzazi(Baba/Mama) au ndugu(kaka/dada) na rafiki hakikisha unawafunza mipaka kati yao na yenu wazazi na pia marafiki zao na usichoke kuwakumbusha mara kwa mara au pale inapohitajika.
5-Utaratibu wa kula na kulala, inategemea na malezo/makuzi nyumbani kwenu, hiyo pia ni sehemu ya Kacha hivyo ni muhimu kuifuata kama ilikuwa reasonable mf: sisi tulikuwala x3 kwa siku na muda wa kulala ilikuwa saa mbili na nusu na watoto wakubwa ioikuwa Saa tatu na nusu. Ijumaa na JMosi ni flexible kwa wote ila usipitilize zaidi ya saa nne.
6-Imani ya Dini(rudi namba moja), najua wengi wetu tumeachana na Dini na badala yake tunaamiji Mungu tu. Kumbuka uamuzi huo umekuja baada ya kupewa nafasi ya kujifunza kuhusu Mungu, kuomba/sali n.k. hii ni nzuri sababu inawapa watoto the Most high wa kuongea nae unapokubwa na jambo maishani, wakati wewe mzazi upo mbali au umeenda busy.
7-Thamani ya Mwili: Bila kujali jinsia, kuwa wazi kuhusu vialevi, mavazi ila sasa sio ndio uwalazimishe wavae kama Wasabato wakati wewe baba yao kutwa upo online unaangalia mapicha watu wamevaa next to nothing. Sio tu kwamba itawafanya wasikie aibu bali wanaeza kuwa target ya kuwa-bullied.
Kumbuka watoto wako wana Asilinya kibongo, tayari wapo tofauti...hakikisha unaitumia tofauti hiyo kuwafunza wanao waitumie kama prevelege. Kuanzia nywele, rangi ya ngozi, u-biligual,u-multicultural na kama under 18 basi u-duo citizenship
Nitakuona kesho. Bai..
Comments