...wale wa Miaka 30-39, isipokuwa mimi ambae naelekea miaka 50 na wanangu wala hawajafika miaka 16. Hawa teen ndio wanaoendesha Social media huku kaka/dada zao in their 20s wanasakama watoto wangu(kizazi kipya aka kizazi cha mwanzo).
Nilienda kuchukua mwanangu wa Sekondari nakutana na wamama watu wazima...mie pia ni mtu mzima ila naona kama vile wenzangu wazee zaidi yangu kwa muonekano, makunyanzi na mvi...oh bila kusahau fashion.
Talking about fashion, siku moja kabla ya Covid19 my Std 5 kid akanambia "kwanini unapenda kuvaa same dark colors "clothes" nikamwambia navaa different colors but Winter coats ndio the same dull colors....halafu ikawa March 2020(deleted memories).
Anyways, turudi kwenye malezi ya watoto wenu wanaosumbua mitaa ya social media na real life.
Wengi ambao wapo in their 30s(kwa mujibu wa hiyo comment) bado ni Wanawake wa nguvu na waliamua kuwa na watoto bila Baba kwasababu wanaweza kufanya kila kitu wenyewe, na Wanaume Rijali waliotaka kuacha "alama yao" Duniani.....sasa wamefika umri wamegundua wanahitaji penzi, companion, mwenza wa kudumu ili ku-share hii life na wakid wao.
Watoto wanakua haraka na kuanza kujitegemea, wakigonga miaka 16 inakuwa kama hawakuhitaji wewe kiviile, unagundua ile "mwanangu wananikamilisha" ni ulongo.
Nature inachukua mkondo wake, ulalo umekujaa mpaka kwenye kope, ile Dildo, Mkono na PH haina love wala warmth ya real man/woman unaanza kusaka penzi....penzi la kweli ni gumu kupatikana, na utu uzima wako unaanza kutoka na huyu, chat na yule, meet na huyo. Hapo hapo kuna kusaka pesa, kulipa bills, kujitunza, n.k...unasahau mwanao ni 16yr na anakuhitaji japo sio kiviiile ila bado ni mtoto na anakuhitaji.
Teenage wanaachwa huru na kulelewa online ya Dunia nzima, unakumbukanule usemi "usipofunzwa na mamayo, utafunzwa na Ulimwengu"? Ulimwengu ndio Internet sasa. It's scary out there.
Huwa nawarahisishia wanangu kuelewa hatari ya kutumia Mitandao ya Kijamii kwa kusema, if I let you go to George Square on your own, will you feel safe? Wanajibu "no, too any people we don't know"....nawaambia the Internet is x 10milioni* bigger than George Square, kuwa in the Internet is equivalent to being on the world with no parents's guidance or protection.
Piga marufuku watoto wako wasitumie Mitandao ya kijamii mpaka angalau wafike miaka 18? God help us!!
Takuona kesho, Bai.
Comments