Mambo?
Aah mie pia nimekukumbuka ndio maana nimeamua ku-blog kila siku mpaka siku ya Christmas. Tegemea michapio kadhaa, nita-edit baada ya Xmas.
Now that is out of the way....njoo kwenye Somo la leo ila kama umekuja kujua namna ya kurudia mwili wako baada ya kuzaa, Pole ila usiondoke nataka nikupe siri yake ili ukome kutaka ku-bounce back haraka haraka, sio tu kwamba ni Kacha ya kimagharibi bali pia ni aina ya unyanyasaji wa jinsia kutoka kwa Mumeo.
Maisha yangu yote nilikuwa chikonda aka skinny hivyo nilijizoea hivyo na nilijipenda nilivyokuwa. Baada ya kushika Mimba kwa mara ya kwanza nilinenepa na nilipojifungua mwili ukarudia wembamba wake ila nikawa "shapely", kwamba nikawa na umbile la kike(vitu vikajitenga, nikatokelezea)zaidi. Hiyo ilichukua wiki 2, Mimba ya pili nikanenepa tena na mwili ukarudi ulipokuwa ndani ya miezi 2...baada ya hapo mambo mengi yakatokea kwenye huu mwili(story ndefu na sina muda) then akaja mtoto mwingine, tufanye wa mwisho....huyu sasa ikachukua miaka 4 (hihihihi) na sijawa skinny tena ila sio Ndimbo(kibongr) pia.
Kwa bahati nzuri suara la mimi kurudia mwili wangu kabla ya mimba na uzazi ni langu binafsi na sio kulazimishwa na mume wangu.
Hivi majuzi kati katika mizunguuko yangu nikakutana na stori ya "Ballelina farm", dada wa miaka 33?(sina hakika) na ana watoto 8 chini ya miaka 12. She looks so skinny, kabla sijamaliza kushangaa nikaambiwa Wiki kadhaa baada ya kujifungua mtoto wa 8, kabla hata damu ya uzazi haijakata, Dada Balelina farm akaenda shindana Miss nini sijui na akashinda.
Nikajiuliza Mama wa nyumbani with 8 kids + baba yao anapata wapi muda na ngugu za kufanya mazoezi? Nikakumbuka watoto 8 na house work zinaweza kufanya usahau kula au upoteze hamu ya kula. Came yo find out the Husband pushed her to keep her skinny body sababu ni sehemu ya beauty standard, pia ana dada wa kazi na wasaidizi kadhaa na zaidi ya yote sio mama wa nyumbani sababu anafanya kazi na kuuza bidhaa kutoka shambani kwake...oh na Mumewe ni Trust fund kid, kwamba they are loaded aka it's cool to be a famer if your husaband is filthy rich....aah nimetoka nje ya topic ila sio mbaya ujifahamu.
Mkasa huo ukanikumbusha wanawake wengi wa mitandaoni na wale mastaa, wanapenda sana kuonyesha miili yao wiki chache baada ya kujifungu. Almost wote wanasukumwa na waume zao na hutishiwa kuachwa ikiwa hawatorudia miili yao kabla hawajashika mimba na kuzaa.
Baadhi wanatoka kwenye Dhehebu la Dini ambalo linaamini kuwa ukiachika watoto wako wanabaki na baba yao na wewe huwezi kwenda Mbinguni bila watoto wako(kitu kama hicho).
Kwa wa Bongo wa mitandaoni lakini wanaishi Bongo huwa wanapenda kuiga au tuseme ku adopt Culture za kimagharibi na utakuta vijana wengi wanaanza kusahau "beauty standards" za Culture zao hasa zile za Kikabila, wanaanza kuhapia kuwa "mke wangu akizaa halafu hakondi, namuacha"...bila kujua kuwa mwili kujirudia pre-mimba inategemea hiyo mimba yake ya ngapi(kama alitoa 3 kabla ya hapo good luck), gene, complications za ujauzito na uzazi husika n.k. uzazi sio lelemama kama mnavyochukulia, ukimaliza ujauzito salama na ukajifungua bila shida na ukapita wiki 12 bila issue. Mshukuru Mungu, hiyo haina maana uzazini rahisi. Uzazi ni kati ya uhai na kifo chako au mtoto au wote.
Anyways, Mitandao imetusogeza karibu na kurahisisha mawasiliano na hivyo tunajua/fahamu mambo mengi mazuri, mema na yale ya kishetani. Tunajifunza ujuzi na aina mbali mbali za maisha ya watu na tamaduni zao. Hiyo haina maana sisi kama wabongo, tuache tamaduni zetu na kudharau beauty standards za Kiafrika na kuchukua za Magharibi.
Beauty standard ya waafrika kiujumla bila kujali nchi Mila na Desturi ni Mwanamke mwenye mwili(sio ndimbo), mwenye haiba ya kike(msafi,anajipenda, msikivu,anajisitiri,anajiheshimu, mwenye kujiamini n.k).
Huko magharibi tuuchukue Elimu. Ufundi, Teknolojia na namna ya kuboresha systems za Serikali(Uchunu, Elimu na Afya) kuboresha maisha ya wabongo bila kubadili utamaduni wetu na viwango vya uzuri.
Nakusikia unauliza, vipi kuhusu wanaume?
Wanaume hawashiki mimba na obviously hawazai, so akibadilika itakuwa ni sababu ya uzembe, maradhi, uvivu au vyote. Kwa ufupi huitaji kushinda gym unless unataka ku-vutia wanafunzi au wanaume wenzio...wanawake wengi bila kujali Tamaduni na Utaifa hatuhitaji kuona umejazia sababu hiyo inamaanisha kiungo muhimu hakipati nafasi ya kufikia potential length muda ukifika.
Takuona kesho, bai.
Comments