Skip to main content

Posts

Showing posts from April, 2016

Jipe Changamoto Deilee....

Mambo? Kama ni mfuatiliaji(mshiriki) kwenye mambo mbali mbali yanayoendelea Online iwe ni kutoa Misada kusaidia wengine, kuhamasisha juu ya Afya, kuelimisha wengine kuhusu issue mbali mbali za Kijamii na hata yale ambayo ni Binafsi. Utagundua kuwa hayo niliyoyataja hapo juu huwaunganisha watu wote na kuwa kitu kimoja kwenye Suala husika linalofanyika kwa Wiki/Siku husika, Pamoja na kuungana huko bado hutokea kutofautiana na kutokana na "utoto" wa baadhi basi kufarakana hujitokeza na hivyo kufanya baadhi kutengwa, semwa vibaya  hali inayopeleka wengi kuogopa au kukwepa "kushiriki" kwenye hayo mambo ambayo baade hutumika kusuta wengine.....hukufanya hivi tulivyo fanya vile, halafu leo kimbelembele....si unajua? Sasa ikiwa wewe ni kama mimi(sio mtu wa Drama) na hupendi kujionyesha au hutaki watu wakujuuuuuuue, yeah naandika mengi kuhusu mimi (Kila kitu Mie...got it?)lakini bado hunijui amini nakuambia hihihihihi. Anyway kama wewe upo kama Mie utakuwa na ile ta

Wanaume hawajui kunung'unika/kukaa na Kinyongo....

....Sosho Midia si imewabadilisha? Hakika bado wapo hivyo ila namna wafanyavyo ni tofauti na walivyokuwa wakifanya kabla ya Sosho Midia(nionavyo mimi). Unakumbuka ulipokuwa mdogo(au ni mimi tu), Baba yako akisikia jambo kutoka kwa Mwanaume mwenzie halizungumzii ila anakwenda kwa huyo Mtu na kuzichapa/kumkung'uka Magumi? well Baba yangu alikuwa mtu Mwema na Mtu wa watu lakini alikuwa Ngumi Mkononi, anakutandika halafu yanaisha. sasa hii ndio "Wanaume hawakai na Kingongo" niijuayo mie. Niliendelea kuona hiyo  kwa Kaka zangu na rafiki zao pia na hivyo kuweka Sementi kwenye hilo. Siku hizi Waanaume, wanaanika mambo ya wenzao nje (mitandaoni)ikiwa wamekorofishana, kwamba mmoja akiudhiwa/kasirishwa na mwenzie basi Jamaa wa Shosho Midia wote watajua. Kwa sisi Wanawake ambao hufikiria baada ya action(sio kabla) na kisha kuomba msamaha baada ya kuharibu ni Kawaida(ilizoeleka hivyo), lakini sio kwa Wanaume. Sio kwamba  nasikitika kuwa Wanaume wamebadilika na wala s