Monday, 20 June 2016

Kufanya Mapenzi(Ngono) Hakujengi Ndoa yenye Furaha......


....lakini ni "Madhara" ya Ndoa yenye Furaha! Nimekuchanganya si eti? hata mie sielewe nilichoanza kuandika ila endelea kusoma na mimi niendelee kuandika na kwa pamoja tunakuwa kwenye Mstari na hivyo sote kuelewa. Hujambo lakini?Ngono au Kufanya Mapenzi(kama tunavyopenda kuita sie tulio Ndoani ili kuhisi "Utakatifu" wa Ndoa zetu) sio Muhimu kiviiiiiile, Muhimu ni kutunza au kuendelea kuwa na  ile hali ya kuvutia/vutiwa na Mwenza wako. Kwamba, sasa ni Miaka 8 ya Ndoa yenu lakini bado unapata misisimko uleule uliokuwa ukiupata pale anaposema "kesho nakuja"....tofauti sasa unajua anarudi saa ngapi nyumbani kwenu....Sauku ya kumuona inakupa tabasamu kuu.Wakati mwingine Unajiambia/jisemea ni jinsi gani unampenda Mume/Mkeo bila yeye kukusikia. Wakati mwingine wala huamini kuwa unaishi na Mwenza umpendae hivi(japo huwa anakuudhi na unamnunia)....Ukimuona Mkibaba unahisi "kunyetukanyetuka" na yeye akisikia sauti yako  Mkimama basi tena hana Hali. True Story!! turudi kwenye Topic......Ngono (Kufanya Mapenzi) ni Madhara ya Ndoa yenye furaha.....unajua, kila kitu kina Faida na Madhara yake si ndio? Sasa faida za Ndoa zipo nyingi lakini Ngono(kufanya Mapenzi) sio moja wapo. Kufanya Ngono(Mapenzi) ni Madhara ya kuwa na Ndoa yenye furaha. (Hiki kipengere kimejirudia....Usijali, kuandika na kueleweka sio kazi rahisi kama udhaniavyo)!


Kwamba, ni lazima Madhara hayo yakupate ikiwa Ndoa yako imesimama Imara na imejawa/egemea Upendo, Furaha na yale yote Mema mlioelekezwa, funzwa, jifunza n.k. Pamoja na kusema hivyo bado Ngono(kufanya Mapenzi) haipaswi kufanywa Kila siku. Ikifanyika kila siku inapoteza "Mngaro"? hihihihi mnapoteza "ubunifu" a.k.a mnaishiwa!..........ndio hiyo inatoka kwangu Mie yule wa Enzi pale Dinahicious, ambae nilikuwa nawashanga sana Watu wanalala vipi Kitanda kimoja bila kupandana kila siku angalau Mara 3. Achana na hili. Mnapokuwa kwenye Ndoa mambo mengi hutokea, kumbuka mmeunganisha Familia mbili tofauti. Kila familia hukutwa na issues zake ambazo huwahusisha ninyi pia kwa pamoja. Kwamba likija kutoka kwenu ni lake  na likija kutoka kwa Mumeo pia ni lako. Ukiachilia hayo kuna Malezi ya Watoto na Majukumu Mengine kibao ya Kimaisha.Sasa mnapoishiwa "Mngaro" au Ubunifu ni wazi kuwa mtakuwa na kazi ya ziada ya kutafuta mambo Mapya ambayo katika hali halisi ni yale yale tu sema hamjayafanya kwa muda Mrefu, but Muda wa kufikiria on how to actually do it tena unagharimu kwani tayari Masaa 24  yapo full....ni kama vile hayatoshi.Hivyo ni Muhimu kufurahi pamoja bila kukutanisha Miili nakufanya Mapenzi Daily(mara 3-4 kwa Wiki inatosha), kama bado au  ulikuwa hujui basi jaribu kujifunza  kuwa karibu nae:-

1)-kuonyesha Mapenzi kwa Vitendo popote mlipo bila kuingiliana, Busu, shika/gusa kwa Huba, Mahaba yaani kuwa "Intimate".

2)-Kiroho-kujadili Imani yenu/zenu na Kusali pamoja.

3)- Kiakili-Kufanya Mazungumzo ambayo hayahusiani na Watoto/Kazi/Ndugu.

4)-Ongezea as you go.....Mpaka umefika hapa ni matumaini yangu kuwa umenielewa au tumeelewana. Kama bado basi usisite kuni-Tweet nami nitafanya Blog Post ingine Spesho kwa ajili yako.


Nathamini Muda wako mahali hapa na Ahsante sana kwa kuichagua Blog hii.

Babai.

Sunday, 19 June 2016

Toto Baya, Zuri kwa Mama(au a face only Mother can Love)....

...sio kila Mtoto huzaliwa Mzuri, na karibu Watoto wote (hasa wanaozaliwa Kiasilia) hutoka wamevimba-vimba kama Kiazi Mviringo. Wale ambao huchelewa kutoka au Wale ambao Mama zao hujizuia wasiwazae(sukuma) Garini/Chooni ndio huwa Balaa(wanatisha hihihihi)! Mtoto anatoka, wanakukabishi u-bond nae lakini wewe unamrudisha chap-chap kwa Daktari/Mkunga kisha unaanza kulia. Ile kulia baada ya Kukamatishwa Mtoto ile huwa ina Siri zake, sio furaha tu!Kibibi soon after Birth....0 Day old!Wanangu wote walipozaliwa nili-share Picha zao za Masaa Machache tangu kuzaliwa, sikuonyesha Miguu wala Mikono kwa kisingizio cha "Privacy" zao, nilikuwa Aware Wanangu wamevimba-vimba ila ile hali ya Kujivunia mimi kuwa Mama ndio ilinisukuma ku-share Pics za awali kabisa tangu wazaliwe.....Privacy wakiwa wamevimba-vimba alafu wanapoteza "Privacy" wakifikisha Miezi Kadhaa? Sema tu ukweli tu kuwa katoto kako kabaya  hihihihihihi and it's okay! it's Nature!!
Babuu alipozaliwa alitokea poa tu, hakuwa Kavimba wala nini hehehehe ila Kibibi sasa....eeeh alitokea kama "Small Potato" sijui Homono?...kwa kawaida inamchukua Mtoto Siku 3-28 "kunyooka", kuwa kawaida(Chunguza zile Sherehe Asilia za Saba na Arobaini ya Mtoto kwa undani utaelewa kwanini)...Saba Mtoto anatoka kushikwa na Wanafamilia, Arobaini anatoka Nje rasmi na tayari kukutana na Shida za Mtaa/Dunia.

Kibibi 3Months oldKwa Ughaibuni ya England ni tofauti, Watu tunaenda Shopping day 5(actully sio Shoppng ni Check ups)....wengine Manguli wajitoa same Day. Ile katoka Hospitali tu unamkuta Coffee Shop (Ruksa kushangaa na kucheka)!Mara nyingi mtu anapata Hatia kusema "katoto kako kabaya", anaishia tu kusema "awww she/he so cute",,,sasa ukisema hivyo na wakati Mie Mama mtu najua Kichanga wangu kavimba-vimba nitakukata jicho ambalo litakufanya ubadilishe Sentensi yako kutoka "she/he is Cute" to "she/he looks like you both" which sio rahisi....nani anafanana na Wazazi wake wote? Zaa uyajue na kwambia!Safari apitiayo Mtoto ndani ya yale Masaa Machache ya Uchungu kuanza kushtua mpaka unapochanganya, Maji kumwagika na wewe Kuanza Kusukuma ni ngumu....achilia mbali "stress" unazompa pale unaposema umechoka au huwezi tena kusukuma!! Hivyo usitegemee Mtoto kuzaliwa "Mzuri".Suala muhimu ni kwa Mtoto kuzaliwa Salama na mwenye Afya, Pia wewe Mzazi kumaliza safari hiyo salama(kuzaa is Next to Death). Suala la "Uzuri" wake litajulikana huko mbele na ata-deal nalo mwenyewe bila Msaada wako.


Ahsante kwa Kuichagua blog hii, Nathamini Muda wako hapa.

Babai.

Thursday, 2 June 2016

How to(Jinsi ya) kumheshimu Mumeo...


...muendelezo wa Post ya jana, kama hujaiona bofya hapa. Najua ungependa kujua namna ya kumheshimu Mumeo zaidi badala ya kuwa Chini yake si eti? Kama ujuavyo sote tumepetia Mazingira/Malezi/Makuzi tofauti na hivyo hatufanani Kitabia, hivyo basi Kuheshimu Mume nijuavyo mie huenda ni tofauti na ujuavyo wewe.,...sasa labda chukua ambalo ulikuwa hulijui na ongezea kwenye yale uyajuayo? au acha kama yalivyo ila ukiweza share yako na mie "niangalizie".Kumbuka Heshima ni muhimu kwa pande zote mbili lakini leo tunaegemea kwa Mwanaume kwasababu mimi ni eerrrr Mwanamke? also Topic ilikuwa Mwanamke kuwa Chini ya Mwanaume? Sasa kama tumeelewana hapo, twenzetu;Muachie maamuzi Makubwa-Hata kama Kipato chako ni Kikubwa mara Nane kuliko chake, Sio unajiamulia tu kununua Nyumba au kupeleka Watoto Private School kwa mfano..... kwasababu tu unaweza. Mpe Mumeo nafasi na mjadiliane. Unaweza kuweka Mezani aina/sehemu 3 za Shule/Nyumba na kisha muache yeye afanye Uamuzi wa Mwisho kisha mpe-support. Baadhi ya Wanaume ni wazito kwenye Utendaji na kuna namna ya kukabiliana na hili,  ila sio kufanya maamuzi Makubwa kisha unampa ripoti ya nini ulichofanya.Salamu-Kwasababu tu mmelala pamoja na hukuhisi akigalauka Usiku haina maana alilala vizuri na kumbuka usiku ni Mrefu...pia hamkuwa wote Ndotoni. Kama mlivyokuwa enzi zile kabla hamjafunga Ndoa eeeh! umeamkae leo mpenzi....well sio lazima useme hivyo, Mambo?, Umeamke? Upo okay? etc! Pia katikati ya siku akiwa kwenye mishughuliko yake na atakapowasili Nyumbani.
Shukuru-Pamoja na Usawa wenu bado Mwanaume huwa na Presha kubwa ya kulinda na kutunza Familia yake. Onyesha shukurani kwake kwa yote afanyao kama "mwanaume". Kushukuru hapa kupo kwa aina tofauti sio lazima useme "ahsante Mume wangu kwa kuwa mwanaume wa nguvu/kweli" bali unaweza kusema zaidi kwa vitendo(nitaandika Post inayojitegemea kwenye hili...nikumbushe au vipi?).Pia ni muhimu kumshukuru kwa lolote analokufanyia hata kama ni dogo, Mfano kaamka leo na kasafisha vyombo....mwambie ahsante. pengine kawahi kuamka na kuwaandalia watoto Kifungua kinywa lakini kaenda tofauti na utaratibu uliowawekea watoto na hivyo kuharibu utaratibu wa siku nzima.....mshukuru tu hivyo hivyo.....hihihihihi!Jijali/Jipende/Jirembe-Sijui wale  "napenda Nachuro" nafasi yao ipo wapi Mbinguni? ila ni muhimu sana kujipendezesha na kuonyesha kuwa unajijali kwa ajili ya Mumeo. Ikiwa wote ni Wafanyakazi  nje ya Nyumbani basi Mkimama jitahidi kuwa unawahi nyumbani mapema kabla yake ili upate muda wa "kujiweka sawa" kwa ajili yake. Kupendeza kwako  sio tu kutakufanya ujisikie Vizuri kama Mwanamke pia ni wazi kuwa kutaonekana kwa Watu wengine na hivyo Mumeo kuonekana kuwa anajua kutunza Mkewe.....hii kwa baadhi ni Heshima kwao!Uliza kabla ya Kukosoa-Hasa kama Mnawatoto au Mnabiashara pamoja  au vyote. Kuna sababu kwanini kafanya alichokifanya hivyo basi kabla ya kuanza kumkosoa ni vema kuuliza kwa upole kwanini kitu fulani kimefanyika ili upate kuelewa na hivyo kutafuta ufumbuzi kwa pamoja. Epuka kukosoa-kosoa mara kwa mara!Usimseme vibaya/Mshushua-Mbele ya rafiki zenu, kuna wakati Mumeo anaweza kuteleza/lopoka mbele ya Rafiki zenu kwenye Party au mkusanyiko wowote.....lolote lililomtoka muunge mkono  na kuwa upande wake(bila kusema neno). ikiwezekana kuwa sharp ku-justfy (muokoe kutoka kwenye kujiabisha).....mkifika nyumbani ndio umuweke sawa. usimuweke sawa mbele ya watu wengine no matter how close you are with those watu.Usilalamike au kunong'ona-Kama kuna kitu Kikubwa kafanya hakijakupendeza, tafuta muda weka issue Mezani muijadili kwa upole na Upendo. Vitu vidogo vidogo kama vile Kunya/Kojoa pembeni ya choo(yes some Mumes still do that), kutosafisha bafu baada ya kuoga au kutoweka kitu mahali pake...sio kwamba anafanya hivi kwa sababu wewe ni "kazi ya Mwanamke" bali hivi vitu sio Muhimu kiviile kwake(inategemea na Malezi). So rekebisha na move on au mwambie moja kwa moja ili aache habits hizo.Mhusishe kwenye  Utaratibu wa Siku wa Watoto-Mama ndio huwa Mstari wa  mbele kuweka Sheria, Kuweka Ratiba, Kuweka utaratibu n.k. katika harakati za Malezi na kurahisisha Maisha, mara nyingi Baba huwa Kazini akifanya yake ya Kibaba ili kuweza kutunza familia yake. Hivyo kupitwa na yote uliyoyaweka ambayo wewe na Watoto mnayafuata ili kurahisisha Maisha ya kila siku ni rahisi.  sasa ni muhimu kumhusisha Baba ili ajue yote yanayoendelea. Sio mara zote atapatia lakini itakuwa rahisi kumuweka sawa ikiwa tayari ulikwisha muelezea utararibu wa siku wa watoto. Wakati mwingine watoto watamwambia "Mama hafanyi hivyo, Baba umekosea"!!Muandalie Chakula aka "umtengee" mara nyingi,  natambua kuna zile siku ambazo unakuwa hoi na yeye anaelewa kuwa umejichokea na hivyo anaingia mwenyewe Jikoni na Kujipakulia. lakini jitahidi kuweka chakula tayari kwa ajili yake.


Usikivu-Mumeo anapozungumzia issue muhimu  ya kifamilia (hata kama mwanafamilia wake humpendi) au pengine adha alizokutana nazo Kazini, msikilize kwa makini bila kumkatisha au kuonyesha kuwa haupo inteested.Usimuingilie kwenye Muda wake na Watoto-Hii ni ngumu(nakwambia kama Mama), lakini ni lazima ujifunze kutoingilia afanyacho Mumeo  kwa Watoto wenu so long  hakihatarishi Maisha yao Kihisia au Kisaikolojia...maana some Babaz nao huwaga wapuuzi, hupenda kuogopwa rather than kuheshimuwa na watoto. wanadhani ni sifa!


Uelevu kwenye "Hadithi" zake- Inaweza kuwa Siasa, Uchumi n.k....chochote ambacho kinam-interest. Jitahidi kumuelewa na ikitokea huelewi  mahali ni vema kuuliza kabla hajaendelea ili arudie tena kuliko kujifanya umeelewa halafu uulize tena mbeleni wakati alichokuwa akikielezea kimekaribia Mwisho....hii hukatisha tamaa na kuonyesha kwamba ulikuwa hausikilizi na hivyo  kuua "stimu" ya Hadithi.
Omba Ushauri na wake-Ikiwa kunajambo ungependa kulifanya na huna uhakika, kabla ya kuomba ushaurii kwa shoga zako au Mama/ndugu zako....Muombe yeye kwanza!
Epuka kulimbikiza Makosa ili Kumsuta- Mwanaume kama Mwanaume, usipoliweka wazi Kosa lake linapojitokeza basi ndio imetoka hiyo....ama hajui kama amekukosea au anasahau. Sasa  ukitokea Mzozo na wewe ukayaingiza yote hayo kwake inakuwa kama vile unamsuta kwa Makosa ambayo hayajui(yapo kichwani mwako).
Usiingilie Ugomvi wake- Kabla Era ya Sosho Midia haijajulikana wengine hapa tulifundwa kuwa tusiingilie Ugomvi kati ya Mume na Ndugu zake, na badala yake kuwa "sikio" na usikilize....akiomba ushuari basi shauri kwa makini na hakikisha ushauri wako haukandamizi upande wa Pili ambao ni Ndugu zake. Kuwa upande wake lakini pia kuwa Fair, kwani hao ni Ndugu na wewe ni Mwanamke tu(Ouch)!!


Sasa Era hii watu na wake zao wanafuatana humo Sosho Midiani, time to time Mume anaweza kupishana na Mtu/watu.....ikawa ngumu kwako kama Mke kushuhudia Mumeo akiwekwa Konani. Jitahidi usiingilie, mwache amalize Ugomvi wake mwenyewe!Kwa leo wacha niishie hapa, Tambua nathamini Muda wako hapa na Ahsante kwa kuichagua Blog hii.

Babai!

Wednesday, 1 June 2016

How to(Jinsi ya)...kuwa Chini ya "Mumeo"....


....imekuwa kawaida kwa Wanandoa Wake kwa Wame kutafuta "jinsi ya" kufanya mambo mbali mbali ili kuifanya Ndoa kusimama Imara na kuepusha misuko-suko ya kihisia na hivyo kupelekea Ndoa kuwa Ndoano na pengine kuharibika.


Hii kuwa "chini ya Mumeo" hata mie siijui na vyovyote ilivyo kamwe sitokubali kuwa "Chini" ya  Mtu yeyote achilia mbali Mwanaume ila nitakuambia ninachokijua ambacho huenda ni tofauti lakini bado kinamrudishia Mwanaume hali ya kujihisi/sikia kuwa anaheshimika/heshimiwa na Mkwe.Tatizo kubwa linalofanya Wanawake kukumbushwa au lazimishwa na Jamii kuwa ni LAZIMA wawe chini ya Wanaume (asiwe na Sauti) pale wanapoamua kufunga Ndoa ni kutokana na Imani kuwa Mwanamke anaposimama na "kujitetea" na/au kum-challenge Mwanaume basi huesabika kuwa hana Adabu, hana Heshima kwa Mwanaume husika.
Ukweli ni kuwa unapokuwa kwenye Ndoa ya "ndio Bwana"  kwamba kila anachokisema Mwanaume wewe unakubali tu....huondoa Changamoto na hivyo kufanya Ndoa kuwa a bit "boring" na ni wazi kuwa hautofurahia Ndoa hiyo kwa sababu hautokuwa na Sauti,...Ndoa inaendeshwa na Mtu mmoja, kwamba kuna maamuzi yatakuwa yakifanywa na Mumeo ambayo wewe hupendezwi nayo lakini kwa sababu ya "Uoga" aka kuwa Chini yake ambako wewe unadhani ni "heshima" unaendelea kuwepo humo.
Ikiwa unatoa "Heshima" huku unahasira au  Moyo/Roho inakuuma ujue hiyo sio Heshima bali ni "Uoga" ambao ukiendelea utakusababishia Matatizo ya Kiakili na Kisaikolojia(bila wewe mwenyewe kujua), utaishi kwenye Ndoa kwa sababu ya kufurahisha Jamii/Famili/Ukoo na sio kwa ajili yako na Mumeo na pengine Watoto kama mtaajiliwa.Huenda ukawa unamalizia "machungu" yako kwa...labda Msaidizi wako,Marafiki zako au Watoto. Unaweza kuwa mwenye hasira kwa watu wengine ambao hawahusiki.....unatoa Sauti/unakuwa juu huko kwasababu huwezi kufanya hivyo kwa Mumeo. Hivyo unaumiza watu wengine wasio na hatia kwa Upumbavu wako wa kuwa Chini ya Mumeo kama sehemu ya Kumheshimu!!
Ndoa ni Muungano wa Watu Wawili, Wewe na Mumeo. Msingi wa Ndoa yenu unatakiwa kuwa-based na kuendelea kujengwa na pande zote....baadhi ya Mafunzo kutoka kwenye Imani za Dini yamepitwa na Wakati, ni vema kutumia Common Sense rather than kufuata "Mafunzo" ambayo ni Radical na zimeegemea kwenye Mfumo Dume zaidi na kutokana na Maisha yalivyo sasa ni kama vile baadhi hazileti maana? Kwamba tunakabiliana na changamoto tofauti na zile za Miaka 2000BC.
Sasa Heshima kwa Mwanaume ndio sababu kuu/pekee ambayo husababisha Wanawake waambiwe/lazimishwe kuwa Chini ya Mwanaume. Kama nilivyokusia hapo juu, Kuheshimiwa kwa Mwanaume  ni Muhimu sana kama ilivyo kwetu Wanawake kwenye kujaaliwa,kulindwa na kupendwa (kuwa cherished).Nnachojaribu kusema hapa ni kuwa, huitaji kuwa Chini ya Mwanaume! akifanya ujinga muweke sawa ila sio kwa Kumfokea bali kuwa-firm.....kwamba aone kuwa unachosema hutanii na  hutaki mchezo...upo very serious.


Chagua Maneno ya kutumia, ikiwa unahitaji muda kufikiria, jipe muda na tafuta nafasi uwakilishe Issue inayokusumbua. Ikitokea kitu na kinahitaji mabishano basi Bishana kwa heshima bila kutoka nje ya Mstari wa Heshima na kutumia maneno machafu/kashfa..Mara nyingi Wanaume huchukia ikiwa wewe Mwanamke unaonekana "smarter" kwenye Mambishano yenu na ili kukunyamazisha hukimbilia kutumia Kashfa au maneno machafu yatakayokuumiza hisia, sasa hata kama yeye atayatumia bado huitaji kumrudishia hapo kwa hapo. Ugomvi ukiisha/poa muelezee hisia zako za kutokupendezwa na matumizi ya maneno Machafu/Mabaya/Matusi.Kuwa Chini ya Mtu yeyote sio rahisi, achilia mbali Mumeo, mie binafsi siwezi na sitokaa niweze na Yaye Mume wangu analijua hilo....sitaki/sipendi ujinga(naturally mie ni Mkali), nina hoji kwenye kila jambo/kila kitu ambacho kinagusa Familia yetu na hasa Watoto wetu....nadhani hii ni kutokana na sehemu ya "career" niliyopitia? sijui!!Ndoa ni Kazi ya kila Dakika, Kila saa na Kila Siku, ukiwa mvivu basi utakimbilia "mwanamke lazma awe chini ya Mumewe"....acha Uvivu, do your Job! Kama huna Muda wa kufanyia kazi basi usifunge Ndoa....Ndoa haihitaji wavivu.


Usikose Post ijayo ya "Jinsi" ya kuonyesha Heshima kwa Mumeo. Nathamini na Kuheshimu Muda wako hapa, ahsante kwa kuichagua Blog hii.

Babai!