Thursday, 18 August 2016

Jinsi ya kumfanya Mumeo kuwa kama "Romeo" kwa Juliet.......sio kiviile ila close(I promise)....Jello!

Kama Jojoba ni Hohoba kwanini Hello isiwe Jello?
Ni kawaida kwa wengi kutafuta "namna ya" kupenda, kuridhisha, kuonyesha mapenzi, kujali n.k. Kuna siku Mtu aliniuliza  afanye nini ili Mumewe amuombe radhi? nikashangaa...kuna watu hawajui kuomba Radhi Wenza wao?Hakika hakuna Kanuni kwenye Maisha ya Ndoa  lakini kuna yale mambo "basic" ambayo ni lazima kila mtu ayajue na kuyafanya/tenda. Mambo hayo huwa tunafunzwa tukiwa angali wadogo, tukianza Shule na kuendelea kuona Wazazi na watu wetu wa karibu wakiyatenda/fanya . Bila kusahau kutukumbusha pale tunaposahau kuyafuata/tenda/fanya. Ndio maana siku zote huwa nasema kuwa Mwenza ulienae hivi sasa ni Matokeo ya Malezi/Makuzi yake  bila kusahau Mazingira aliyokulia. Kiongozi kwenye Malezi hayo mambo huwa ni Mama (au Msaidizi mwenye Values kama wewe au bora Zaidi) kwavile ndio huwa anakaa na Mtoto kwa muda mrefu kuliko Baba.Sasa pamoja na kuwa wengi wetu  hutegemea/dhania kuwa Kila Mwanaume ni lazima awe "loving" kama "Romeo" kwa Juliet, kwamba anakuambia anakipenda mara kadhaa kwa siku kwa aina tofauti ya Maneno, mkiwa mtaani anapachika Mkono kiunoni, anakupandisha garini kabla yeye hajapanda, anakubusu mara kibao kwa siku, anafanya Ngono Kiromansi mara zote mnapohitajiana...Romeo huyo hakulelewa kwenye Mazingira yale yale aliyolelewa Mumeo. Romeo ni yeye na Mumeo ni Mumeo.Suala muhimu hapo ni kwako wewe kumjua  vema Mumeo kabla hajawa Mumeo, vilevile ni kwako wewe kuwa wazi kwake(usi-settle for less ila usiende overboard)....kama kuna mambo hawezi/hajui kuyafanya na sio muhimu sana kwako basi achana nayo. Mf;- Kutolewa nje kwa jili ya Mlo, Yeye kuosha Vyombo, Kukuimbia, kusema "honey i am hooooome" hihihihi. Kuna yale muhimu/basic ambayo ni lazima ajifunze kuyafanya hata kama hawezi,  nayo ni Heshima, Ukweli, Thamini, Shukurani na Kuomba Msamaha/radhi. Ikiwa Mumeo kabla hajawa Mumeo na hujamuweka sawa kwenye hayo basi Ndoa yako itakuwa Chungu...utahisi kuwa Ndoa yenu ni ya Mtu mmoja na utakuwa Mpweke Ndoani. Utahisi kumpenda Mumeo lakini hutopendezwa nae Siku 305 kati ya zile 365 za Mwaka!....je unaweza kuishi na Mtu anaekuudhi kwa Muda huo wote wa Maisha yako?Sie wa "kizamani" tulifundwa kuwa Mke anaweza kuchukua nafasi ya "Mama" kwenye kumuweka sawa Mumewe, ila sasa unapomfunza Mumeo yale muhimu ambayo Mama yake  labda hakutilia maanani hupaswi kuwa kama Mama yake kweli na yeye kuwa Mtoto  wako bali unapaswa kufikisha "Somo" kivingine ukijitumia wewe kama mwenye hitaji la "tabia njema" kutoka kwake Mumeo Mpenzi.Ninachojaribu kusema hapa ni kuwa Wanaume hawafanyi mambo yale yale ambayo wewe unadhani ndio Kupendwa na  kwamba kila Mwanamke  anapata "Tamu" ya "Romeo" kwa Juliet. Kuna Wanaume ni Wapenzi wazuri sana lakini hawajui kusema "Nakupenda" kila siku, hawajui kusema "samahani/nisamehe" kila wanapokukosea, hawajui kuwa Romantiki.....wana namna zao tofauti-tofauti za kufikisha ujumbe kuwa wanakupenda, wanaomba msamaha na kuromantika.Siwajui Wanaume wote Duniani ila "I lived" hihihihi so nitakupa Uzoefu wangu. Tafadhali usikose kunitembelea tena ili ujue ni namna gani hasa baadhi ya Wanaume hufikisha ujumbe uleule wa kiRomeo bila kuwa kama Romeo.


Nathamini na kuheshimu Muda wako hapa, ahsante kwa kuichagua Blog hii.

Babai.

Thursday, 11 August 2016

Kukabiliana na Mwenza/Mpenzi "mpya" baada ya Miaka kadhaa...


....kwa maana ya yeye kubadilika/shwa na "Rafiki" zake kama niliyogusia Post iliyopita, ikiwa hukuisoma basi bonyeza hapa. Upo salama lakini?....twenzetu!


Kwanza kabisa usimwambie kuwa umebadilika, lakini akikujia na mambo mapya ambayo awali hakuwa akipenda/fuatlia then hoji kulikoni? mf: tangu lini Mpenzi unatazama Eastenders? Hee siku hizi unafuatilia hiki/kile? hii itamfanya atambue kuwa unaona mabadiliko.Pili, Jiweke mbali, yaani mbaaaaaali na hao/huyo "Rafiki" unaedhani ana/amembadilisha Mwenza/Mpenzi wako. Usimuulizie, akianza kukupa stori bila kutaja jina la Mhusika, wewe sema tu "tunamzungumzia John"(taja jina la huyo rafikie mpya)? Halafu onyesha kuwa huna "interest" ya kujua zaidi.(hii itafikisha ujumbe na hivyo kuacha stori za huyo mtu/watu).Tatu, Ataanza kutaka kukutanisha wewe na huyo "Rafiki" kwa kisingizio chochote tu, kuanzia "ametualika kama familia" au "anataka kuja kututembelea ili awaone watoto/apajue Nyumbani". Weka Mguu chini na mtolee Nje kwa upendo na upole kwa kumwambia kuwa Mpenzi/Mume wangu....vyovyote unavyomuita. Ashura ni Rafiki yako, mmekutana Kazini na nafurahi umejenga urafiki na mtu Mahali pa  Kazi. Ila ni vema kama ukitenganisha Maisha yako ya Kazini na ya Nyumbani.Hapa lazma atabisha kwasababu atakuwa tayari kaongea na kumhakikishia "Rafiki" yake kuwa atakwenda  na Familia/Mke/Mume wake, sasa ili asimuangushe ni wazi atakubishia na hata kuonyesha Ukali na kukufanya ujisikie kuwa hupendi watu, atasema hakuelewi, atasema umebadilika na mengineyo basi tu kukuuudhi ili umkubali. Usi-panick. Tabasamu na Mwambie haupo Comfy  kukutana na Mtu wa Kazini kwake amjue yeye Mumeo/Mkeo/Mpenzi wako huko na sasa amjue Nyumbani pia.Ongeza kwa kusisitiza (ukiwa firm bila kufoka) kwamba  huyo ni Rafiki yake yeye na sio Rafiki wa Familia yenu hivyo basi ni muhimu ya Kazini yabaki huko na ya Nyumbani yabaki Hapa(nyumbani). Kama ni muhimu sana na hutaki kumuangusha rafiki yako, basi nenda mwenyewe. Mimi na Watoto(kama mnao) hatuhusiki na urafiki wako wa Kikazi.Nne, Mwambie mwenza wako kuwa ni vizuri kutengeneza Marafiki lakini ni vema zaidi ikiwa mtatengeneza marafiki kama Pea nje ya Kazi, kwamba muwe na Marafiki wapya ambao hamkukutana Kazini. kwasababu kuwa na Rafiki anaekujua Kikazi, Kisosho na Kifamilia/Nyumbani ni Hatari na ni Mwanzo wa kutengeneza Adui.Kumbuka, wapo watu wanatafuta Marafiki ili kujenga Uadui  mahali pa Kazi. Utendaji ni Ushindani. Kupata kazi na Kubaki kwenye kazi na hatimaye Kupanda Cheo kunahitaji Ushindani. Ushindani huo unaweza ukawa Mzuri kabisa na ulio-base kwenye utendaji na Bidii yako, lakini pia wapo ambao hupenda njia za Mkato.
Sasa unapoanza Kazi mpya, unakuwa "vulnerable" na hivyo  "maadui" huchukua nafasi hiyo ili waje kukumaliza kirahisi huko baadae. Sikutumi kuwa usijenge marafiki kwa kuhofia wao kuwa Maadui baadae, isipokuwa nasema kuwa ni muhimu Rafiki wa kzini wabaki huko na Nyumbani wawe wengine. Ikitokea Kazini kumebuma, angalau Nyumbani kutakuwa Salama....kwamba  hamtowavuruga Watoto na hakutakuwa na "Mama mbona hatuendi tena kwa akina Peter"?  "Mama naomba kumpigia Simu  Antie Rose". Vilevile Adui hatokuwa na lolote alijualo kuhusu Nyumbani kwako na kulitumia ili kukumaliza zaidi.


Nadhamini Muda wako hapa, ahsante kwa kuichagua Blog hii.

Babai.