Skip to main content

Posts

Showing posts with the label ElonMask

Twitter ya Elon na heka heka zake...

Ni mwaka na wiki kadhaa tangu Elon Musk alazimishwe na "Mahakama" aichukue Twitter  baada ya kutishia kuinunua 2021(for attention) na ni Mwaka  Mmoja na Wiki Sita tangu nami niachane na Twitter(nisome  kama unajali  ). Maisha bila twita yamekua ya kwaida na sijawahi kuhisi kutamani kuchungulia na kusalimia watu wangu ambao huwa  nawakumbuka mara kwa mara na kutabasamu kutokana na vichekesho au jinsi tulivyokuwa tunaelewana, kupishana na kushangaa pamoja. Hey I miss you on twita too. Sasa juzi hapa nikaona habari kwamba Elon anataka kubadilisha Kindenge na kuwa Eksi(huenda tayari imekuwa hivyo), nikaudhika na kuombea Twita ikufe kabisa na kubaki kumbukumbu, maana ni aibu hata kusema niliwahi kuwa Twita tangu mwanzo miaka 17 iliyopita. Ilikuwa jamii nzuri sana na kamwe sitoisahau kama ilivyokuwa DHB(Dar Hot Board)/DHW(Dar hot Wire), JamiiForum na Facebook. Nimesikia kuna mabadiliko mengi ambayo nilijua yatatokea kutokana na jinsi Elon anajibeba. Elon ni Bilionea amb