Ni mwaka na wiki kadhaa tangu Elon Musk alazimishwe na "Mahakama" aichukue Twitter baada ya kutishia kuinunua 2021(for attention) na ni Mwaka Mmoja na Wiki Sita tangu nami niachane na Twitter(nisome kama unajali ). Maisha bila twita yamekua ya kwaida na sijawahi kuhisi kutamani kuchungulia na kusalimia watu wangu ambao huwa nawakumbuka mara kwa mara na kutabasamu kutokana na vichekesho au jinsi tulivyokuwa tunaelewana, kupishana na kushangaa pamoja. Hey I miss you on twita too.
Sasa juzi hapa nikaona habari kwamba Elon anataka kubadilisha Kindenge na kuwa Eksi(huenda tayari imekuwa hivyo), nikaudhika na kuombea Twita ikufe kabisa na kubaki kumbukumbu, maana ni aibu hata kusema niliwahi kuwa Twita tangu mwanzo miaka 17 iliyopita.
Ilikuwa jamii nzuri sana na kamwe sitoisahau kama ilivyokuwa DHB(Dar Hot Board)/DHW(Dar hot Wire), JamiiForum na Facebook. Nimesikia kuna mabadiliko mengi ambayo nilijua yatatokea kutokana na jinsi Elon anajibeba. Elon ni Bilionea ambae anapenda "attention" na ana mashabiki ambao wanaamini kuwa yeye ni JINIASI kitu ambacho kinamfanya awe tofauti na mabilionea wengine, hiyo pia inamfanya aonekane kuwa yupo karibu zaidi na watu wa kawaida(masikini) na "anawajali" kumbe katika hali halisi anachuma kidogo walichonacho hao masikini.
Watumiaji wa Twitter wanamchukulia jamaa kama mkombozi which is sad kwasababu platform ile haimfaidii yeyote bali Elon pekee, sasa anawakomboaje bila ninyi kukomboleka? labda akianza kuwalipa watumiaji wake kwa content creation kama ambavyo Google(Aphabet) anafanya kule Youtube na huku Blogger. Kwamba isiwe micro-blog tena na iwe blog-BLOG na kuwe na video format itakayoruhusu watu wenye utaalam hitajika kutoa Elimu n.k. Kwasasa inaonekana(kwa mujibu wa Mashable) kumejaa soft porno, bulling, exposeeS kama pumziko baada ya stress za siasa na drama za watu kwenye maisha yao binafsi.
Twita ilikuwa na nguvu na kujitengenezea sifa nzuri kwa miaka 17, ilikuwa chanzo cha habari in real time kitu ambacho kilifanya Waandishi wa habari kuitumia kama kituo cha kwanza kutoa dondoo/tip/habaro kwa ufupi nahivyo wananchi kwenda kwenye News paltform kupata habari kamili. Pia ilikuwa ni kituo kizuri kwa wanaharakati na bila kusahau ilikuwa sehemu ya ya kufanyia research kwa Content creators wa Maswala ya Siasa kwenye Paltform nyingine kama vile youtube, blogger,facebook na instaglam.
Miaka ambayo nilikuwa na bahati kuitumia Twitter (kutoka facebook 2007) na kuona mabadiliko mbali mbali ambayo yalikuwa bora na baadhi ya kuudhi, twita iliendelea kutamba kutokana na urahisi wa kutoana kupata habari/maelezo moja kwa moja kutoka chanzoni. Tuone Titter ya Elon itadumu kwa Muda gani. Nikiwa mkweli napenda kusem akuwa naombea sana ifeli, sijawahi kufurahia mtu kufeli ila Elon akifeli na Xtwita yake nitafurahi sana. Siku moja nitarudi nione yaliyomo....labla. Mpaka siku hiyo endelea kuwa nami huku kwa Blogger ya Google....namaanisha Aphabet Inc.
Picha kutoka kwa Mashable
Comments