Skip to main content

Posts

Showing posts with the label asilia

Juice na Soda husababisha "Homa" zisizoisha kwa Watoto....

Heri ya Mwezi mpya wa May. Mungu abariki kila jema upangalo kufanya(na-sound kama Pastor sasa eti?)! Umewahi kujiuliza kwanini Mwanao/Wanao huwa na Homa au Vikohozi visivyokwisha? Ukimpeleka Hospitali na kupima Damu na kila kitu majibu ni kuwa hana Malaria wala Typhoid (hatuna huku ila inawezekana ulipo haya Magonjwa yapo) na magonjwa Mengine ya Utotoni. Wahenga...well Bibi yangu alisema "Mwanangu kuwa Uyaone", mie nasema kuwa na Watoto ujifunze! Wazazi wengi huamini kuwa Soda  husababisha  Watoto kuchangamka kupita kiasi na pengine kukosa usingizi, baadhi huamini kuwa hufanya Watoto kuwa na tabia za ajabu(wabishi,wakahidi, hawakusikilizi, wananguvu kupita kiasi) kutokana na Soda ambayo huwafanya kuwa "high". Sasa hizo ni Soda na zina some sort of "hewa" sio, kwamaana hivyo Juice za kawaida ambazo hazina Sukari ni salama(nilidhani) tena zile ambazo unachanganya na Maji(squash) ndio Bora zaidi(nilijidanganya). Kuna wakati tulikuwa tukinunua

Kula Fresh Vs Natural?

Hi.....kwa mara nyingine! Back in 2006 kulikuwa na mabishano kuhusu matumizi ya vitu ambavyo sio asili kwa matumizi ya Mwanadamu. Wengi wetu (tukisaidiwa na chunguzi mbalimbali) tuliamini kuwa matumizi ya vyakula vya Kopo, Madawa ya kutibu, aina za Sabuni, matumizi ya Microwaves n.k huenda ndio sababu ya magonjwa  Mengi yasiyotibika na kuu ni Saratani. Miaka ikapita na tukakugundua kuwa kutokana na Maendeleo ya Teknolojia kwenye kila kitu hakuna u-natural......kwamba hakuna mtu anakula kiasilia kwasababu mazao yote yanakuzwa na Mbolea ambayo ni "man made". Ukiachilia mbali Mbolea ni Maji tutumiayo kumwagilia mimea na madawa ya kuua wadudu wanaoshambulia Mazao.....Umepata idea ya wapi naelekea ambako sitaki kufika(sitaki post ndefu). Bado mabishano yapo au niseme yameamia kwenye utunzaji wa ngozi na Nywele. Watu wanajisifu kuwa wao ni Natural na hawataki Chemical(relaxer) kwenye miili yao lakini bado wanakunywa maji (bombani au chupani yote yanakemikali). Wanatumia Sabun