Hi.....kwa mara nyingine!
Back in 2006 kulikuwa na mabishano kuhusu matumizi ya vitu ambavyo sio asili kwa matumizi ya Mwanadamu.
Wengi wetu (tukisaidiwa na chunguzi mbalimbali) tuliamini kuwa matumizi ya vyakula vya Kopo, Madawa ya kutibu, aina za Sabuni, matumizi ya Microwaves n.k huenda ndio sababu ya magonjwa Mengi yasiyotibika na kuu ni Saratani.
Miaka ikapita na tukakugundua kuwa kutokana na Maendeleo ya Teknolojia kwenye kila kitu hakuna u-natural......kwamba hakuna mtu anakula kiasilia kwasababu mazao yote yanakuzwa na Mbolea ambayo ni "man made".
Ukiachilia mbali Mbolea ni Maji tutumiayo kumwagilia mimea na madawa ya kuua wadudu wanaoshambulia Mazao.....Umepata idea ya wapi naelekea ambako sitaki kufika(sitaki post ndefu).
Bado mabishano yapo au niseme yameamia kwenye utunzaji wa ngozi na Nywele. Watu wanajisifu kuwa wao ni Natural na hawataki Chemical(relaxer) kwenye miili yao lakini bado wanakunywa maji (bombani au chupani yote yanakemikali).
Wanatumia Sabuni na bidhaa nyingine kusafisha nguo na miili yao. Wanakula chakula ready made(kopo au paketi).....wanapaka Manukato na kupaka Vipodozi.
Wanatumia bidhaa zinazorangazwa kuwa ni "all natural" hakuna kinachotengenezwa na kukaa Dukani bila kuwa na "kemikali" ya kusaidia kiendelee kuwa salama kwa mayumizi yako.
"All natural" inalipa lakini haina maana kuwa ni "all" hata kama wameandika vikivyomo kwenye bidhaa hiyo. Kumbuka sio lazima waandike au wakuambie kuwa kuna Asilimia Kumi na Moja ya Kemikali ili kusaidia bidhaa hiyo kudumu kwa muda mrefu.
Sooooo chagua kula Fresh na sio Natural......fanya utakavyo juu ya mwili wako lakini usijitambe(bado mnatumia neno hili?) Kwamba wewe ni "natural" kwasababu hujajichubua au una-rock nywele zako bila kuosha wala kupaka Mafuta(achilia mbali relaxers).
Mie ni mpenzi wa kula "natural" tangu enzi....lakini nikiwa mkweli ni kwamba nimekuwa nakula fresh na sio natural.
Nikuache kwa sasa, ahsante kwa kuichagua Blog hii.......babai.
Comments