Skip to main content

Posts

Showing posts with the label chenchi

Bahili, Mchoyo au Mbinafsi...

Heeiyaaa! Shukurani kwa uwepo wako siku ya leo. Watu wa hivyo tunaishi nao lakini kwasababu tunawapenda(Mapenzi upofu) inakuwa ngumu kujua au kutambua. Hawa bwana wanaweza kukufanya uishi maisha ya kiupweke kabisa na huzuni na hivyo kuondoa maana ya Umoja wenu. Sasa leo nataka ujue kiduchu tu. Wale majaa wanaotaka kujua umetumiaje Pesa na wakigundua umetumia senti kwa matumizi yako binafsi ambayo wao (wanaume) wanaamini kuwa sio muhimu wanaanza kung'aka! Wakati mwingine unaona unaongeza mavazi ya watoto ili wapendeze lakini bado mtu anakuambia "mbona wanakila kitu"....Inafikia mahali unaanza kuhisi kama vile unasimangwa na hivyo unaamua kutumia pesa zako. Akiona Pesa anazotoa zinatumika kwa kile anachodhani au kuamini kuwa ni "muhimu" lakini bado unapendeza na watoto wanapata vitu vipya na vizuri mara kwa mara anaacha kutoa Pesa za Matumizi.....huyu ni Bahili! Mchoyo; Mara zote akirudi nyumbani baada ya Kazi....unamuandalia chakula  anakuambia "nilipi