Heeiyaaa! Shukurani kwa uwepo wako siku ya leo.
Watu wa hivyo tunaishi nao lakini kwasababu tunawapenda(Mapenzi upofu) inakuwa ngumu kujua au kutambua.
Hawa bwana wanaweza kukufanya uishi maisha ya kiupweke kabisa na huzuni na hivyo kuondoa maana ya Umoja wenu. Sasa leo nataka ujue kiduchu tu.
Wale majaa wanaotaka kujua umetumiaje Pesa na wakigundua umetumia senti kwa matumizi yako binafsi ambayo wao (wanaume) wanaamini kuwa sio muhimu wanaanza kung'aka!
Wakati mwingine unaona unaongeza mavazi ya watoto ili wapendeze lakini bado mtu anakuambia "mbona wanakila kitu"....Inafikia mahali unaanza kuhisi kama vile unasimangwa na hivyo unaamua kutumia pesa zako.
Akiona Pesa anazotoa zinatumika kwa kile anachodhani au kuamini kuwa ni "muhimu" lakini bado unapendeza na watoto wanapata vitu vipya na vizuri mara kwa mara anaacha kutoa Pesa za Matumizi.....huyu ni Bahili!
Mchoyo; Mara zote akirudi nyumbani baada ya Kazi....unamuandalia chakula anakuambia "nilipita kwa Jeff (amuuza Kuku wa Kubanika) Mke wangu...usijali" unaishia kula peke yako(wakati ulikuwa umasubiri mle wote).
Unamlalamikia kuwa ni vema akuambie kabla ili usimsubiri na pia asipoteze chakula(sio kila mtu ana Jokofu).
Haya anaacha kula kwa Jeff lakini anarudi na kifurushi cha Mishkaki au chakula chochote "fast" au cha Mataifa mengine( Chinese, British, Indian) for One!
Anakukaribisha ule akijua kabisa utakataa kwasababu hakitoshi kwa watu wazima wawili.....na tangu katoka job lazma atakuwa na njaa so yeah.
Wengine wanapitiliza mpaka kwenye Mavazi na Manukato...kila siku anajininulia yeye tu. Wewe ukienda shopping unamkumbuka.. myeye walaa!
Oh kuna zile simu za Mkataba kwa sisi wa Ughaibuni.....hihihihi yeye amachukua the latest one wewe unachukuliwa the sooo January 2015 aka 2014 smartphone.
Mbinafsi; Mara zote mkienda kufabyavmanunuzi kwa mfano....mkiwa checkout anakutegea.....au anajifanya yupo busy kutafuta Kadi yake....au anaenda kulipa lakini anaweka incorrect pin hahahahha au anakuuliza (bila aibu) unalipa au nilipe?
Huyu mjamaa usipinuomba pesa za matumizi rafiki yangu utakuwa Single Mum with a hubby(napenda hii sentensi).
Wengine tunajitegemea Kiuchumi hivyo hatujazoea kuomba pesa lakini linapokuja suala la matumzi ya familia, mwenza wako hapaswi kuombwa.....anatakiwa kujua kuwa kila Siku/Wiki lazima pesa itumike so wacha Kadi au Chenji/Chenchi.
Halafu kuna wale Wazito kutekeleza....oh hii ni Post kwa siku ingine(ni kikumbuka).
Babai.
Comments