Skip to main content

Mwili ni Mashine....

......inayo-process Kemikali (chakula na mengineyo)....kuna wakati Machine inahitaji "huduma" ili kuendelea ku-process Chemicals ili uendelee kuwepo.


Njia pekee ya wewe kujua kuwa Mwili(Mashine) inahitaji " huduma" no mwili huo kukuambia kwa ama kuumwa au kujisikia ovyo/vibaya.



Hapa sizungumzii kuumwa Magonjwa ya kuambukizwa na Mbu au Virusi (Mafua, Tetekuwanga au hata HIV)au yale ya kurithi kama Moyo, Kisukari n.k.



Kuna watu ambao wanaishi wakitegemea Dawa kusaidia Mashine zao kuendelea kufanya kazi kwa muda mrefu.....kwamba mwili unaposema "mamaa nimechoka nahitaji kupumzika"....mwenye mwili ana pop a Chidonge au Mavidonge.



Celebs wanakuambia ili ufanikiwe unatakiwa kufanya kazi bila kuchoka (wana pop pills hao).....katika hali halisi mtu huwezi kusafiri kila siku na kufanya shows usichoke!



Huwezi ku-pop pills kila siku za maisha yako kwasababu unaongeza Chemicals mwilini na hivyo mwili kufanya kazi ya ziada na hivyo ku-over choka. Nachukua a year off ndio huwa inakuja hapo.


Upatikanaji wa Dawa (happy pills) hizo kwa nchi hizi za mbele umekuwa rahisi hivyo watu wa kawaida pia wanazibugia kwa ifuatavyo.



Anyway.....nachotaka kukuambia ni kuwa naumwa Uchovu kuanzia Unywele kichwani mpaka Unyayoni(sina nywele unyayoni).



Zisi bizinesi ofu being'i a mamu ofu tu anda faivu kidizi in yukei izinti a joki.

Babai.

Comments

Topic hizi tamba...

Weusi wa Kwapa na Vipele Makalioni....

Well Weupe huwa hawawi na weusi kwapani bali Unjano au Ukahawia....wale wenye nywele nyeusi sasa ni another case. Kuhusu Vipele makalioni havina Ubaguzi, raha ya vipele vile ni kwamba havionekani kwa Macho....utajua unavyo kwa kujipapasa, au gusa ngozi yako....inakuwa kama ina "mikwaruzo" wajua ile nanihii ya kupiga Msasa mbao? Yep ndio feels kama hivyo! Usione haya sio Ugonjwa na wala sio Tatizo kiafya, ni mambo ya Urembo tu na yawapata watu mbali mbali Ulimwenguni.....kama urembo sio issue kwako basi baki na Mapele yako na uyafurahie! Mimi nilikuwa nayo na siyapendi na ndio maana nataka nikupe mbinu ya "mapambano" ili uwage na Makalio "smooth"....Sasa hapa nikuambie kuhusu Vipele Makalioni au weusi wa Kwapa?.....Yote? Hamna shida twende in to them*. Vipele: Sijui inasababishwa na nini(sio mtaalam mie) ila nahisi ni kutoijali ngozi ya sehemu hiyo ndio inachangia....huisugui ukioga, huilainishi kwa mafuta, unavaa chupi za Mpira badala ya Pamba, huifanyishi

Kuachisha mtoto Kunyonya!

Heeeeeelp!!! Ka Binti kangu kana Mwaka na Nusu (Miezi18) lakini kamo tu, hata dalili ya kuacha hakana....Mie nimechoka kunyonyesha, nimechoka kuwa Mkubwa hapa Chini ya Kidevu bana! Babuu aliacha mwenyewe ghafla, yaani siku hiyo kaamka tu akagoma kunyonya....Mwanamke bembeleza, lazimisha mtoto wapi!!....alikuwa na Mwaka Moja na Mwezi(Miezi 13) na niliteseka Kihisia na Kimwili kwa Wiki nzima. Kihisia: Haina Uzungu hii, ila nililia sana....kwanini Mwanangu hataki kuwa karibu na mimi? (maana kunyonya kwake kulikuwa kunanipa ukaribu na Mwanangu). Nilipanga kumnyonyesha mpaka Mwaka na nusu (Miezi 18), kwanini Kanigaya(Susa) kabla sijawa tayari?!!! Kimwili: Matiti yanauma bwana asikuambie Mutu! Yalivimba(Jaa maziwa)....the more nakamua ndio yanajaa zaidi.....kamata simu Pigia Mama, Mama akasema "usiyakamue kwani ukikamua mwili wako unahisi mtoto anataka kunyonya zaidi so yanajitengeneza kwa Kasi ya ajabu". Kaongeza: "

Mashoga/Wasenge "wanatuibia" Waume/Wapenzi wetu....

...kwanza kabisa napenda utambue kuwa hakuna Mtu anaweza kumuiba  mwenzake kimapenzi, Mpenzi wako anapotoka kwako na kwenda kwa mwingine ni wazi kwamba kaamua kufanya hivyo, hilo sio kosa lako na wala hujasababisha yeye kwenda huko kwingine bali ni yeye mwenyewe na akili zake timamu kafanya uamuzi huo. Tangu Ushoga ndio khabari/Suala Muhimu wacha na mimi nidaivu ini nipate "trafiki" japo nimechelewa. Tofauti na "platform" nyingine hapa utajifunza kwa kiasi kidogo...au niseme kiasi fulani. Linapokuja suala la Ushoga/Usenge,sehemu kubwa ya Jamii imetawaliwa na  Uoga ambao unapelekea kutokuelewa Ushoga ni nini? Hali hiyo ni Asilia, kwamba mtu anazaliwa hivyo au ni uamuzi  wa mtu au ni Hali inayojitokeza ukubwani baada ya Kubalehe.....pale kijana anapoanza kutambua ujisia wake(je anavutiwa/penda Wanawake au Wanaume au wale wa Jinsi kama yake). Mie sio Mtaalam wa Masuala ya Kisenge/Shoga lakini ni mtu ambae napenda kudadisi, na watu wazuri kuwadadisi ni hao hao