Unashangaa Kijana wa miaka 20na anatumia Cream za mikunjo usoni kuna tofauti gani na wewe(mie) unaetumia za Mature people wakati hata hujafika miaka 40?
Za umri chini ya miaka 60 zinanipa vyunusi bana na nyingine kukausha ngozi kupita kiasi......nilipojaribu za mature people(miaka 60+) sikupata vyunusi na ngozi ikawa na afya njema.
Sio mbaya kuanza mapema kuitunza ngozi yako kwasababu anti-wrinkle actually haziondoi wrinkle(mistari/mikunjo usoni) ila inachelewesha sio?
Sasa kutokana na masitiresi ya maisha bana watu wanapata Mikunjo kabla ya umri. Makampuni ya utunzaji wa Ngozi nayo yanakategolaizi antirinkozi kuanzia miaka 25(well wenzetu Weupe wanakunjika mapema so yeah).
Kwa kawaida Waafrika(Weusi) huwa hatupati makunyanzi mapema na wengi wetu huwa tunaonekana wadogo kuliko Umri wetu.
Aaah! Stori time***
Siku nipo kwa Dentist akaja madada na Pram yake....anaulizwa utambulisho wake (jina na DoB) akageuka kuangalia nani anatilia maanani....akamnong'oneza tarehe akamalizia na 1995.
Ukimuangalia ni mtu mzima wa miaka 40na.....hihihihihi hivi Wazungu hawajui kuwa Weusi(wa Afrika) tunaonekana wadogo kuliko umri sio wakubwa kuliko Umri.
Hata kama unapunguza (najua wengi mmepunguza) basi punguza miaka 2 hadi 5 sio 20 khaaa....huoni aibu?!
Babai.
Comments